MISTARI YA WIMBO HUU

Na na na na
Na na na na
Na na na na

Ni sababu gani mwanitenda hivi
Uwongo mwanena kunihusu mimi
Hamnifahamu hamjui
Chenye nafanya maishani
Mwangu nyumbani
Mwangu nyumbani
Mijidai eti nyie marafiki
Kumbe nia zenu zilikuwa kundi
Kunitenganisha na mpenzi
Wa roho yangu na kuniacha
Mashakani taabani

Ni chuki ndo nahisi
Nikiwaza jinsi
Mlivyojitolea kuniudhi
Bila matokeo yaani
Ni chuki ndo nahisi
Nikiwaza jinsi
Mlivyojitolea kuniudhi
Bila matokeo yaani

Mambo yenu mi sishughuliki nayo
Mnavyoishi mimi sina hoja nayo
Kinachonihusu si lazima
Mkifahamu na kushinda
Mkipiga domo
Mkipiga domo
Mlichotenda kwangu kweli hakifai
Kiwango cha unchungu mlinipa yaani
Sina heshima kwenu tena
Ukuta wa chuki mlijenga
Kati mi nanyi
Kati mi nanyi

Ni chuki ndo nahisi
Nikiwaza jinsi
Mlivyojitolea kuniudhi
Bila matokeo yaani
Ni chuki ndo nahisi
Nikiwaza jinsi
Mlivyojitolea kuniudhi
Bila matokeo yaani

Na na na na
Ni shida kuamini yaani
Na na na na
Kiwango cha uchungu mlionipa
Na na na na
Heshima kwenu mimi sina tena
Na na na na
Basi chuki ndio mimi nahisi

Ni chuki ndo nahisi
Nikiwaza jinsi
Mlivyojitolea kuniudhi
Bila matokeo yaani
Ni chuki ndo nahisi
Nikiwaza jinsi
Mlivyojitolea kuniudhi
Bila matokeo yaani

Toa Maoni Hapa

SHIRIKISHA MWINGINE

Your email address will not be published. Required fields are marked *

SHIRIKI KUONGEZA MISTARI

VIDEO YA WIMBO HUU