MISTARI YA WIMBO HUU

Daka kamba twenzetu tusonge na wanetu
Tusifuate wachache wanaoua ndoto zetu
Tuna mipango yetu
Tuna baraka zetu
Tuna misingi yetu
Tunaishi ndoto zetu

Daka kamba twenzetu tufungue wanetu
Tuachane na hao wanaoua bara letu
Tuko na mali zetu
Tuko na mila zetu
Tuna akili zetu
Tuko barani kwetu
Daka Kamba

Wananiona Prophet najiona Poet
Since way then nadondosha tu ma’project
Daka kamba maskini unaeteseka
YES nikufute chozi kabla hujawa mateka
Na hizi code zinavuka mipaka waliyoweka
Moja kwa moja jua yatima huwezi deka
Daka kamba twenzetu uliyedhulumiwa
Haki na bado skendo ukaumbiwa
Ushindi waja tena bila kuhadithiwa
Niko mbali na siasa chafu “zingatiwa”
Daka kamba wajawazito kijijini
Usisubiri baiskeli ikufikishe mjini
Sipendi kuona ukijifungua njiani
Damu uhai vinakupa mtihani
Daka kamba tusogee hadi mbele
Tujue nini shida ikibidi iwe kwele

Daka kamba twenzetu tusonge na wanetu
Tusifuate wachache wanaoua ndoto zetu
Tuna mipango yetu
Tuna baraka zetu
Tuna misingi yetu
Tunaishi ndoto zetu

Daka kamba twenzetu tufungue wanetu
Tuachane na hao wanaoua bara letu
Tuko na mali zetu
Tuko na mila zetu
Tuna akili zetu
Tuko barani kwetu
Daka Kamba

Peke yangu sitaweza beba dunia begani
Kwa pamoja tunaweza kumshinda shetani
Tukapange mikakati tukutane makantani
Mabadiliko yaanze nami kila siku niko vitani
Unajua nini maana ya uafrika wako leo
Unaukimbiaje ukweli kwa kuzidisha vileo
Afrika ya kila kitu vipi tukose maendeleo
Ungana nasi tuushinde ukoloni mamboleo
Usikate tama kuna siku tutafika
Kimbia ujinga jitambue kisha wajibika
Udadisi ndio mwanzo wa kuelimika
Tukikosa maarifa Afrika wanatuzika
Gaddafi RIP fikra zake zidumu
Simameni acheni kulaumu
Kwa maarifa nifuate jisafishe utakate
Mafanikio hayaishii kupata pesa ya mkate

Daka kamba twenzetu tusonge na wanetu
Tusifuate wachache wanaoua ndoto zetu
Tuna mipango yetu
Tuna baraka zetu
Tuna misingi yetu
Tunaishi ndoto zetu

Daka kamba twenzetu tufungue wanetu
Tuachane na hao wanaoua bara letu
Tuko na mali zetu
Tuko na mila zetu
Tuna akili zetu
Tuko barani kwetu
Daka Kamba

Yeeah
Umoja ni nguvu
Waafrika Amkeni
Yeah
2015
Adamoe
Lugombo
Oldpaper
Daka Kamba

Toa Maoni Hapa

SHIRIKISHA MWINGINE

Your email address will not be published. Required fields are marked *

SHIRIKI KUONGEZA MISTARI