MISTARI YA WIMBO HUU

The time is now it’s gonna be ugly in a minute
The time is now it’s gonna be ugly in a minute

Samahani mami naomba dakika yako moja tu
Nataka kuongea mimi nawe
Nijibu nifurahi, uonekane unajidai
Naomba na namba yako ntakucheki baadae
Samahani mami naomba dakika yako moja tu
Nataka kuongea mimi nawe
Nijibu nifurahi, uonekane unajidai
Naomba na namba yako ntakucheki baadae

Nataka nikueleze mapenzi niliyoyafuga enzi
Ujilambe masikio kwa asali za Tanga hizi
Raha zinaanzia hapa na hizi sioni zikiisha
Taratibu kama Taarab, njoo madini ntakulisha
Sina ugeni wa mapenzi, ni mgeni wa mapenzi yako
Ndo maana nakupiga mkono niombe japo minute yako
Hata aliyebuni gari alishakufa kwa ajali
Kwa hivo sioni ni hatari kukuachia moyo kamili
Kila siku ni ka birthday yako, meno yanaumana
Mishangazo asubuhi ndo mapenzi yameungana
Keep the romance alive kama ndo kwanza nakuona
Mapenzi hayatapungua, kesho yake ntakupenda sana
Nishajivika kitanzi, njoo mama ufyatue kiti
Namaanisha biashara please niamini kama benki
Mwanamke kweli kwa definition ya mtogwa kote
Sio lazima nikutongoze, macho yangu yashasema yote

Samahani mami naomba dakika yako moja tu
Nataka kuongea mimi nawe
Nijibu nifurahi, uonekane unajidai
Naomba na namba yako ntakucheki baadae
Samahani mami naomba dakika yako moja tu
Nataka kuongea mimi nawe
Nijibu nifurahi, uonekane unajidai
Naomba na namba yako ntakucheki baadae

Nakupenda na unajua naumia, baby
Ndugu zako wanajua navyojisikia, mamaa
Wanawake mko wengi, ndio, zaidi ya mia, baby
Lakini kwako nimeapa nitatulia, mamaa

Shaka ondoa, sikufati kwa ubaya
Kuwa huru nami sitakuhisi vibaya
Muonekano wako ndo umeyazua haya
Yessaya!
Mapenzi hayafichiki kama mwanga kwenye giza
Niache nikuzibiti sina nia ya kukuumiza
Mengi mema tuna-wish ila si kukupoteza
Heya, don’t think I’m a player, sitaki kukuchezea
Watu wangu wa nguvu hamuwezi kuamini kwa penzi
Nimezama ndani nasaka madini
Mtoto mwenye mvuto napenda unavyojiamini
Niruhusu mami niwe wako tuanze share maishani
You told me unapenda my style na sina papara
Of course, napenda your style na huna shobo hata noti
Sihitaji tu game, sihitaji tu-fling mi na we
Mi nahitaji tu-fame, tukiwa na wheels

Samahani mami naomba dakika yako moja tu
Nataka kuongea mimi nawe
Nijibu nifurahi, uonekane unajidai
Naomba na namba yako ntakucheki baadae
Samahani mami naomba dakika yako moja tu
Nataka kuongea mimi nawe
Nijibu nifurahi, uonekane unajidai
Naomba na namba yako ntakucheki baadae

Dakika moja tu, mimi nawe
Niseme seme nawe, na kama muda hautoshi
Basi naomba namba yako ntakucheki baadae
Ntakucheki baadae, ntakucheki baadae

Toa Maoni Hapa

SHIRIKISHA MWINGINE

Your email address will not be published. Required fields are marked *

SHIRIKI KUONGEZA MISTARI