MISTARI YA WIMBO HUU

Dar es Salaam Temeke Ilala Kinondoni
Hii ni yetu sote
La mgambo lishalia eh kijana mwenzangu oh

Mm-mzee wangu
Hata wewe mdogo kwangu
Tusafishe mazingira kwa afya yako na yangu
Dar Es Salaama jiji langu
Mvua ni kazi ya Mungu
Hapo hapo ulipo safisha mazingira yako
Uwe gado
Ah yaiyaa eh
Hapo hapo ulipo safisha mazingira yako
Uwe gado mama maa

Ule usemi unaosema
Kila uchafu wa mbele yako
Ni mali yako ondoa
Dar Es Salaam tufanye usafi eeh
Temeke tufanye usafi eeh
Tandale tufanye usafi eh
Kilungule tufanye usafi eh
Nnavyokupendaga ehh
Wewe usafi eh
Unavyong’aa ng’aa kwenye madisco mpaka nadataga eh

Mama Shabani ebu fanya utoke
Bwana Makonda eh
Anataka usafi eh
Iweje umalize kula ndizi utupe ganda barabarani?
Iweje eh unachafua jiji?

Mkao mkao mkao wa kula jiji la Dar Es Salaam
Tumempata kijana mwenzetu mwingi mwenye nidhamu
Mkao mkao mkao wa kula jiji la Dar Es Salaam
Tumempata kijana mwenzetu mwingi mwenye nidhamu
(Makonda)
Usafi kwanza
(Makonda)
Yee yeiyee
(Makonda)
Safisha jiji baba eh
(Makonda)
Wanao tupo nyuma yako baba
(Makonda)
Tusafishe jiji baba Makonda

Simu ninunue Tandale nikapige selfie Oysterbay
Wapi na wapi
Kwanini nisifanye Tandale iwe safi kama Oysterbay
Ni shing ngapi
Bora kutembea kumenifunza eh mie
Kutembea kumenifunza
Watu miji yao wanaitunza baba
Miji yao wanaitunza Paul Makonda

Kijana we sharobaro unavyopendeza safisha na jiji lako
Ili ufanane nalo oh (ili upendeze)
Si kutupia viwalo mazingira yako unayotoka doro
Kwepana na jambo hilo oh
Jua kwamba ah ni burudani iih
Jiji langu Dar Es Salaama likiwa ng’aring’ari eh
Usiwe mzuri wa sura
Mavazi pia tabia
Wanakusifu sana eti mtaalam wa kuchana jeans
Uchafu
Hauuoni
Uchafu
Hauuoni
Wanakusifu sana eti mtaalam wa kuchana jeans

Masela ehh
Majita ehh
Mzazi kasema tufanye usafi tuunge mkono
Nangu nangu bila andonya
We shoga ake mama umeniona
Ah nangu nangu bila andonya
Ah shoga ake mama umemuona (anafanya usafi huyo)

Mkao mkao mkao wa kula jiji la Dar Es Salaam
Tumempata kijana mwenzetu mwingi mwenye nidhamu
Mkao mkao mkao wa kula jiji la Dar Es Salaam
Tumempata kijana mwenzetu mwingi mwenye nidhamu
(Makonda)
Usafi kwanza
(Makonda)
Yee yeiyee
(Makonda)
Safisha jiji baba eh
(Makonda)
Wanao tupo nyuma yako baba
(Makonda)
Tusafishe jiji baba Makonda

Hapo hapo ulipo safisha mazingira yako
Uwe gado
Ah yaiyaa eh
Hapo hapo ulipo safisha mazingira yako
Uwe gado
Mama maa aah

Dar Es Salaam tupende usafi eeh
Magufuli kataka usafi eh
Wanafunzi tupende usafi eh
Makonda kataka usafi eeh

Toa Maoni Hapa

SHIRIKISHA MWINGINE

Your email address will not be published. Required fields are marked *

SHIRIKI KUONGEZA MISTARI

VIDEO YA WIMBO HUU