MISTARI YA WIMBO HUU

Mimi ni msanii (mimi ni msanii)
Kioo cha jamii (kioo cha jamii)
Mimi naona mbali (mimi naona mbali)
Kwa darubini kali (kwa darubini kali)

Mimi ni msanii (mimi ni msanii)
Kioo cha jamii (kioo cha jamii)
Mimi naona mbali (mimi naona mbali)
Kwa darubini kali (kwa darubini kali)

Afande anasema wote (wote kimya)
Ntakayo nena hapa yatamgusa mwenye hekima
(Hapo!) hapo ulipo
Kama waipenda pepo kwanini uogope kifo?
(Eehee) unachekesha
(Aah) wanipa raha
Unafikiri mbinguni utakwenda kwa motor car eh?
(Ama utapata zali kama Yesu alivyopaa?)
Acha kujidanganya, kwa Mungu si kwa mzungu
Unapokwenda kwa pipa ikibidi kwa njia za panya
(Loo) haiwezekani
(Hasa?) bila ya imani
Unaelipiza baya kwa jema…
(We ni shetani)
Haufai kanisani, haufai msikitini
Na hutufai kwenye fani
Take care utapotea
(Aliwazalo mjinga ndilo litalomtokea)
Na hii ndo darubini (darubini)
Wasanii muweke akilini, hasa kwa mtu makini
Makini kiusanii
Ila kama mtalii (no sweat, tupa kapuni)
Watakuokota chini
Unafanya mziki Bongo unaekti kama matoni
(Ya nini?!)
Bora kuimba katuni
Lugha ngeni za nini kwenye mziki wa nyumbani?
(Wakati Bongo Flava inapeta zaidi uswahilini)
Mi n’nacheka sana (hee)
Kuna vitu vya kuimba vyenye maana kila kona
(Sasa?)
Inakuwa vipi unataja taja majina tu, nyimbo nzima
(Tena) kwa mistari isiyo na vina!

Mimi ni msanii (mimi ni msanii)
Kioo cha jamii (kioo cha jamii)
Mimi naona mbali (mimi naona mbali)
Kwa darubini kali (kwa darubini kali)

Mimi ni msanii (mimi ni msanii)
Kioo cha jamii (kioo cha jamii)
Mimi naona mbali (mimi naona mbali)
Kwa darubini kali (kwa darubini kali)

Yes, naona mbali, kwa darubini kali
Ndo maana mziki wangu unaegemea kwenye ukweli
Kwa mfano…
(Labda ungewapo mfano kabla hujashusha kibano)
Nasema rap ni ukweli mtupu, rap jasiri
Rap si kuimba uongo (kama siasa za bongo)
Useme kwenu una Benz wakati jumba la udongo! Mh!
Bwa’ mdogo acha upambe, unavyopelekwa tu
Unakwenda kama ling’ombe
(Simama utupe ujumbe)
Kama huwezi unyamaze
Nasema mara ya mwisho…
(Sio lazima wote tuimbe)
Watu wanataka ujumbe, sio majigambo tu
(Mnasifu ngono na pombe)
Pumbavu hamna soni eh, kwenye zama za ukimwi
Kwenye nchi masikini, ya pili kutoka chini
Afande nashangaa (hata Mungu anakataa)
Kwa msanii wa nchi hii
Kuimba nyimbo za furaha, kila saa
(Wakati huko kijijini watu wanakufa kwa njaa)
Haipendezi, kutomjali mwenzako eti kwa ajili ya mavazi (haipendezi)
Ama kujiona bora eti kwa ajili ya makazi (haipendezi)
Kuna tofauti gani kati ya Temeke na Mbezi?
Au labda ukiishi Mbezi utakapokufa hauozi? (twashangaa)
Eti Majani vipi? Kwanza stopisha beat
Nimuulize kijana alichokipata ni kipi
Aliponyoosha miguu wakati blanketi ni fupi
(Aling’atwa na mbu kwenye visigino huyo)

Mimi ni msanii (mimi ni msanii)
Kioo cha jamii (kioo cha jamii)
Mimi naona mbali (mimi naona mbali)
Kwa darubini kali (kwa darubini kali)

Mimi ni msanii (mimi ni msanii)
Kioo cha jamii (kioo cha jamii)
Mimi naona mbali (mimi naona mbali)
Kwa darubini kali (kwa darubini kali)

Na bado tu, mwaka huu haki ya nani
Mamluki kwenye game mtatoka taka msitake
(Na hii ndo maanake)
Mwanamke kama hataki basi muache aende zake (usimbake)
Kulazimisha penzi ni hatari sawa na kulazimisha fani
(Kisha unaleta utani)
Mpumbavu, hilo ni kosa kama padri kubaka muumini
(Au kama ticha mkuu kumbaka denti ofisini)
Utafungwa! (arabuni utanyongwa)
Bwa’ mdogo, ndani ya shamba la miwa hauwezi ukavuna miogo
(Kuna tofauti kubwa kati ya wivu na usongo)
Sahau superstar, superstar
Kujifanya msanii ndani ya jumba la sanaa
(Wasanii tunashangaa) unashuka si tunapaa
(Unainuka si tunakaa)
Ukipotea? (Kwetu furaha)
Adui? (Muombee njaa)
Ntanyoosha mikono juu hata kama alikuwa shujaa

Mimi ni msanii (mimi ni msanii)
Kioo cha jamii (kioo cha jamii)
Mimi naona mbali (mimi naona mbali)
Kwa darubini kali (kwa darubini kali)

Mimi ni msanii (mimi ni msanii)
Kioo cha jamii (kioo cha jamii)
Mimi naona mbali (mimi naona mbali)
Kwa darubini kali (kwa darubini kali)

Toa Maoni Hapa

SHIRIKISHA MWINGINE

Your email address will not be published. Required fields are marked *

SHIRIKI KUONGEZA MISTARI