MISTARI YA WIMBO HUU

Yeah
Moja kwenye beat
Naitwa Songa eeh
Noma Records
(Sauti za Busara)
Shout-Out to ID
(Six Illmatix)

Nikisema amani iwe nanyi haimaanishi isiwe nami pia
Nafika napo kwenda japo sitazami njia
Haki inaniambia
Sio rahisi kuipata wakimbizi kambi wanaikimbia
Watu wanaruka bila bawa
Wanatengeneza ugonjwa wakijua watauza dawa
Naweka chakula nawa ukishindwa kula gawa
Kiongozi wa nje kura ya mzawa
Naambiwa mengi kuliko ninayoyaona
Kwamba walio macho wachache kuliko wanaokoroma
Wanaugua ugonjwa ambao usio pona
Hata wakiamua kuchana vizibao huwezi shona
Kutokuwa na akili ni pale unapoamua kupenda uoga zaidi kuliko ujasiri
Hata asiye na mabega anabeba begi
Sa hata huoni hatari kwa afya je nani analeta fegi

Watu wanacheza rough ingawa mchezo afya
Hii sio demokrasia ni demoghasia
De-mo-ghasia De-mo-ghasia
Watu wanacheza rough ingawa mchezo afya
Hii sio demokrasia ni demoghasia
De-mo-ghasia De-mo-ghasia

Eyo ndani nina giza we ndani una mwanga
Mi napaa bila nguvu za giza ndani ya mwanga
Je utapaa bila utundu wa visa ndani ya kiwanja
Itakuwa miujiza kuwa na amani bila ya mkwanja
Au ukikua unajiona mjanja
Kumbe ni mshamba na tunajua vipi utapandwa
Utamwagiliwa hapa utapaliliwa pale
Na mwisho wa siku utatoa pamba
Tutavaa na tutajiona kwamba
Tuko safi mithiri ya nyoka aliyetoa gamba
Hali ni ngumu utaisoma namba
Uchungu zaidi ya Sadam alivyonyongwa kwa kwamba
Kunyongwa kwa ganja
Ama sista duu aliye katikati ya matozi na kutoa mlio wa kujamba
Hali ni ngumu mjomba anatamba
Nakupa maneno ambayo umeomba bila kiganja

Watu wanacheza rough ingawa mchezo afya
Hii sio demokrasia ni demoghasia
De-mo-ghasia De-mo-ghasia
Watu wanacheza rough ingawa mchezo afya
Hii sio demokrasia ni demoghasia
De-mo-ghasia De-mo-ghasia
Watu wanacheza rough ingawa mchezo afya
Hii sio demokrasia ni demoghasia
De-mo-ghasia De-mo-ghasia
Watu wanacheza rough ingawa mchezo afya
Hii sio demokrasia ni demoghasia
De-mo-ghasia De-mo-ghasia

Yeah S-O-N-G-A
Songa
Demoghasia
Yeah Kalulete
One The Incredible
Noma Records
Thank you yeah

Toa Maoni Hapa

SHIRIKISHA MWINGINE

Your email address will not be published. Required fields are marked *

SHIRIKI KUONGEZA MISTARI