MISTARI YA WIMBO HUU

Aah dunia
Bado nikiza, bado nikiza
Na marashi ya dunia siyasikii
Najihisi nipo kuzimu naishangaa sayari hii
Iliyojawa wanasiasa, michezo na wasanii
Najiuliza wamekuja huku kutalii
Au wameshahamia dunia ndo haijirudii
Mara nasikia swali kama la nguvu za hoja
Dandu ananiuliza albamu zinajikongoja
Vipi mmegonga copy chini ya milioni moja
Jibu zinalipa sio moja kwa moja
Steve 2K anauliza bifu zinaendeleaje
Nimesha msamehe Casto ameshatoka Segerea
Namjibu bifu lipo na vita vinanyongea
Casto bado anaoza, tuanzeni kumuombea
Complex naye anauliza albamu ile ya wagosi
Walishagonga kopi ngapi hadi sasa kwa wadosi
Namjibu tangu ufe mambo yote ni mikosi
Makundi yanavunjika duniani tunakumiss

Yee iye iye eh
Dunia mapito jamaa
Tuwaombeeni waliokufa wende salama
Mi nawe tupo hatujui siku yetu lini
Kinachotakiwa tuishi kwa amani duniani (mi na wewe)
Yee iye iye eh
Dunia mapito jamaa
Tuwaombeeni waliokufa wende salama
Mi nawe tupo hatujui siku yetu lini
Kinachotakiwa tuishi kwa amani duniani

Kulia nafuta chozi, kushoto lanidondoka
Nakosa raha TX Moshi nikimkumbuka
Muone ananiuliza muziki wa dansi ndio ushashuka
Jibu bado upo, ila naamini pengo lako halitozibika
Mara kwambali nasikia sauti ya gitaa
Sauti ya gitaa inapigwa huku inaniita
Kumbe mzee wakale, hayati Bob Marley
Ananiuliza mziki wa Reggae unaenda vipi
Reggae bado ipo
Ziggy na Damian na Jissy wanagonga copy
Marijani, ananiuliza muziki wangu unaimbwa sana duniani
Vipi familia yangu inafaidika kitu gani
Jibu mimi sina labda mwanao Marijani
Kiza ni kinene sioni pa kupapasa
Mara kwa mbali nawaona wanasiasa
Machozi yananitoka, chini nadondoka
Namuona Karume na Nyerere Julius
Wananiuliza muungano je una nafasi
Nawajibu msiwe na wasi
Sasa ari mpya, nguvu pia na kasi
Ulimwengu mmeuacha dunia ndio inawamiss

Yee iye iye eh
Dunia mapito jamaa
Tuwaombeeni waliokufa wende salama
Mi nawe tupo hatujui siku yetu lini
Kinachotakiwa tuishi kwa amani duniani
Yee iye iye eh
Dunia mapito jamaa
Tuwaombeeni waliokufa wende salama
Mi nawe tupo hatujui siku yetu lini
Kinachotakiwa tuishi kwa amani duniani

Toa Maoni Hapa

SHIRIKISHA MWINGINE

Your email address will not be published. Required fields are marked *

SHIRIKI KUONGEZA MISTARI