MISTARI YA WIMBO HUU

Asubuhi kumekucha Ali naamka
Nakwenda shamba kutafuta matunda
Good mornie sweety ye nakuaga bibie
Nakwenda shamba chochote tutapata
Tutakapo kosa leo mamii tuvumilie
Uh ni Mungu kapanda yote ni matokeo
Ona unavumilia namshukuru Mola
Kote nimezunguka wewe ni mke bora
Ona unavumilia namshukuru Mola
Kote nimezunguka wewe ni mke bora

We hivyo vyote maa (ulivyo)
Nakupendaga (ulivyo)
Dunia ni king’amo dunia mashindano
We hivyo vyote maa (ulivyo)
Nakupendaga (ulivyo)
Dunia ni king’amo dunia mashindano

Mumeo narejea
Hali yangu si waiona
Wakati nakwenda
Ajali nilipata
Ile njia panda nilipita
Alinivamia simba
Na watu wakaja pale kuniokoa
Walinipeleka hospitali ya wilaya
Matibabu nilipata ah
Na sasa nimetoka
Hali yako mjamzito
Usijepatwa mshituko
Dunia ni king’amo
Dunia mashindano
Hali yako mjamzito
Usijepatwa mshituko
Dunia ni king’amo
Dunia mashindano

We hivyo vyote maa (ulivyo)
Nakupendaga (ulivyo)
Dunia ni king’amo dunia mashindano
Hivyo vyote maa (ulivyo)
Nakupendaga (ulivyo)
Dunia ni king’amo dunia mashindano

(Yote ni matokeo)

Ona unavumilia namshukuru Mola
Kote nimezunguka wewe ni mke bora
Ona unavumilia namshukuru Mola
Kote nimezunguka wewe ni mke bora

We hivyo vyote maa (we hivyo vyote maa)
Ulivyo nakupendaga daaa..
Dunia ni king’amoaaa
Jua milele niwe nawe
Nishakutia medani ya chuma

We hivyo vyote maa
Nakupendaga
Dunia ni king’amo dunia mashindano

Ni kingamo mchumba
Kila mtu na yake
Na mila yake mamaa
Duniani kingambo!

We hivyo vyote maa (ulivyo)
Nakupendaga (ulivyo)
Dunia ni king’amo dunia mashindano
Hivyo vyote maa (ulivyo)
Nakupendaga (ulivyo)
Dunia ni king’amo dunia mashindano

Toa Maoni Hapa

SHIRIKISHA MWINGINE

Your email address will not be published. Required fields are marked *

SHIRIKI KUONGEZA MISTARI

VIDEO YA WIMBO HUU