MISTARI YA WIMBO HUU

Niite emcee anayekuna
Rhymes zinawasha kama upupu
Kama utakuwa hujabuma ni vipi utakuwa maarufu
Najituma napakuwa madude ya nguvu
Nashtukia nimekuacha nyuma baada ya kunifanyia ushushushu
Najua roho inakuuma unapokohoa mi sikohoi
Unafuga nguvu kwa vyuma kurap we goigoi
Unazuga una zangu chuma unatuna unavua kikoi
Unaposikia upinzani hakuna unanuna unakuwa hu-enjoy
Napakua nyimbo naingia jimbo kama gaida
Napiga fimbo kiasi kimtindo tu kama kawaida
Eyo jifunze upinzani usitie maguu ndani ya ulingo
Hajui Fid Q ni nani Hautoi nyimbo unatoa jingle
Amani kwa Murder na Stan na wote wanaonijua kiundani
Flani na flani na wale wanaojua ni jinsi gani
Nilipotaabika kabla sijapata mshiko
Kabla sijafahamika heshimika ndani ya Hip Hop
Nikafunika kama auzega aliodazi
Nafarijika kuona mnavyoniona so guys
Lyrics vina vocals touching
Nipo touch first tattoo ma-star wana bahati
Nipo nawe Fid Q flows zangu zinawa-oversize
Hardcore napenda ku-rap shows za night
Mia kwa mia oya waheshimiwa mpo alright
Heheh thank you thank you

Napopita mtaani watoto utawasikia (Fid Q)
Madada zao huwa huniambia (I love you)
Sababu mi ndo mi mi ndo Fid Q mwana aliyejuu
(Niko ndani ya nyumba basi mikono juu)
Mtaani watoto utawasikia (Fid Q)
Madada zao huwa huniambia (I love you)
Sababu mi ndo mi mi ndo Fid Q mwana aliye juu
(Niko ndani ya nyumba basi mikono juu)

Mashairi yanasambaa kila mahali mithiri ya nzi
Yaani kama Mashahidi Wa Yehova na habari ya Mnara Wa Mlinzi yap
Sio machafu mithiri ya mlima wa kinyesi
Isipokuwa mpumbavu maneno yakikuudhi wanyaka wepesi okay
Kuamini ni zaidi ya kukubali kiakili
Ya kwamba mimi ni jasiri wa roho nafsi na mwili
Navunja ukimya mtu mzima nafanya mziki
Siendekezi jina hela ni heshima au vipi
Huwezi ku-roll weed bila zigi
Ukiwa na hamu tumia condoms kujigi jigi
Au sio
Au vipi
Ebwana ndio
Huu mziki hunipa ushindi wa mic tano
Haijalishi we ni mbishi huenda ulikuwa huijui michano
Kwa mfano ukakosa rangi ya kijani
Basi changanya bluu na njano
Amani ya bwana iwe nanyi wenye msimamo
Asante Mungu kwa hii sauti hata viziwi wataisikimo
Vipofu wanaona hata mabubu wataongeamo
Walio maskini kama Matonya watalia machozi ya diamond
Dunia sio uwanja wa mapambano
Muisafishe mioyo na mwili jasiri atimize agano
FidQ.com copy kibao zitauzwa kwa Ma-Mamu

Napopita mtaani watoto utawasikia (Fid Q)
Na dada zao huwa huniambia (I love you)
Sababu mi ndo mi mi ndo Fid Q mwana aliyejuu
(Niko ndani ya nyumba basi mikono juu)
Mtaani watoto utawasikia (Fid Q)
Madada zao huwa huniambia (I love you)
Sababu mi ndo mi mi ndo Fid Q mwana aliye juu
(Niko ndani ya nyumba basi mikono juu)

Akupigae ngumi ya jicho
Na we mpige ngumi ya sikio
Akikuuliza unaonaje na we muulize unajisikiaje
Mayowe ya chura hayamzuii tembo kunywa maji
Ustaa hauji bila skendo haya kila mmoja anaeng’wie
Sisimizi kumuua tembo au nazi kuvunja jiwe
Sisimizi kumuua tembo au nazi kuvunja jiwe
Hata nguruwe huwa ana-swim mbele ya njaa kufa
Vigumu majivu kuwa mkaa ni sawa na kuurudisha muda
Likikatika dole gumba huwezi andika
Ananisikitisha jinsi wachumba wanavyonikonyeza kwenye giza
Napopita mtaani watoto utawasikia (Fid Q)
Fid Q.com Mwanza ndo home
Na madada zao huwa huniambia (I love you)
Kimziki poa kimapenzi wataishia kuniona hivi

Napopita mtaani watoto utawasikia (Fid Q)
Madada zao huwa huniambia (I love you)
Sababu mi ndo mi mi ndo Fid Q mwana aliye juu
(Niko ndani ya nyumba basi mikono juu)
Mtaani watoto utawasikia (Fid Q)
Madada zao huwa huniambia (I love you)
Sababu mi ndo mi mi ndo Fid Q mwana aliye juu
(Niko ndani ya nyumba basi mikono juu)

Toa Maoni Hapa

SHIRIKISHA MWINGINE

Your email address will not be published. Required fields are marked *

SHIRIKI KUONGEZA MISTARI

VIDEO YA WIMBO HUU