MISTARI YA WIMBO HUU

Haki sawa (mitaa inataka)
Haki sawa (mwanafunzi anataka)
Haki sawa (mwalimu anataka)
Haki sawa (mkulima anataka)
Haki sawa (daktari anataka)
Haki sawa (wasanii wanataka)
Haki sawa (wanamichezo)
Haki sawa

Ah
Piga kelele za misaada ita majirani
Nchi ni nyumba ilochomwa na ina watu ndani
Toka upambane, jifungie ufe chumbani
Tuzikane tusilie, msiba msibani
Mwanangu vumilia mwaume hupata juani
Sumu na sukari vyote vinauzwa dukani
Tangaza jukwaani, angaza kizani
Okoa maisha ya kizazi kinazama mtaani
Sio wazima unavyotuona tumeumia ndani
Na ndugu zetu hawajapona, tumlaumu nani?
Lala kitandani, jifunike dua
Ota imani, kesho Mungu atamulika utakuwa mwangani
Labda maumbo, binadamu ndani hatufanani
Tenda wema kumrudisha Kajala nyumbani
Okoa maisha ya wengine yako hatarini
Mabadiliko wa kuyaleta ni wewe na mimi

Mitaa inataka haki sawa
Funga mtaa ita jamaa kuongeza power
Tukisimama pamoja, hawawezi kutugawa
Wimbo wetu uwe mmoja, tunataka haki sawa
Mitaa inataka haki sawa
Funga mtaa ita jamaa kuongeza power
Tukisimama pamoja, hawawezi kutugawa
Wimbo wetu uwe mmoja, tunataka haki sawa

Piga kelele za misaada ita majirani
Nchi ni nyumba ilochomwa na ina watu ndani
Wingu nzito la mvua limetanda angani
Cha kuvaa umefua unangoja chumbani
Ule wimbo unaokugusa unacheza masikioni
Unavyosikia kama moto umewekwa moyoni
Niko ndotoni, nachoona machoni
Inanipa jibu asiye na dhambi ya kufa utotoni
Moto wa ujana vijana unazidi kuwakolea
Jahazi limezama kina sio cha kuogelea
Maboya wanaelea ila wako pale pale
Mwanaume kufa na kazi, nyumbani wakale
Huu ni muda wa kupata ukipigania
Huu ni muda wa kupambana na kuacha kulia
Mwisho wa kukimbia, ukiwa mnyonge ndo unaumia
Hakuna sifa ya mlevi hazikomoi bia
Ah

Mitaa inataka haki sawa
Funga mtaa ita jamaa kuongeza power
Tukisimama pamoja, hawawezi kutugawa
Wimbo wetu uwe mmoja, tunataka haki sawa
Mitaa inataka haki sawa
Funga mtaa ita jamaa kuongeza power
Tukisimama pamoja, hawawezi kutugawa
Wimbo wetu uwe mmoja, tunataka haki sawa

You know niki-rap mziki wangu huwa naongea kuhusu mtaani
Masikini wenzangu wanaopigana viwandani
Namuhurumia mteja anaejidunga maskani
Watoto wadogo wafanya biashara mabarabarani
Usiku wa manane simu inaita anapiga shetani
Unachekesha unajikuta Mungu samahani
Nawaza mbingu ifunguke kuna siri gani
Furaha ikizidi sana machozi yako jirani
Mvua nyesha utakase kuchafu mitaani
Kila mmoja atakufa, dunia ya nani?
Wasomaji bora msome, mtaani maisha sio club
Majuto asiwe mjukuu unapokuwa babu
Kutafuta majawabu, siri na sababu
Usikate tamaa, nishike mkono nasoma kitabu
Ah Walimwengu, watu na maisha yao
Ukipenda uone milele omba wakupe macho yao

Mitaa inataka haki sawa
Funga mtaa ita jamaa kuongeza power
Tukisimama pamoja, hawawezi kutugawa
Wimbo wetu uwe mmoja, tunataka haki sawa
Mitaa inataka haki sawa
Funga mtaa ita jamaa kuongeza power
Tukisimama pamoja, hawawezi kutugawa
Wimbo wetu uwe mmoja, tunataka haki sawa

Haki sawa (mitaa inataka)
Haki sawa (watoto wanataka)
Haki sawa (walemavu)
Haki sawa (mkulima anataka)
Haki sawa (daktari anataka)
Haki sawa (wasanii wanataka)
Haki sawa (wanamichezo)
Haki sawa (mfanyabiashara anataka)
Haki sawa (madereva)
Haki sawa (kila mmoja)
Haki sawa (Tanzania)
Haki sawa (yeah)

Toa Maoni Hapa

SHIRIKISHA MWINGINE

Your email address will not be published. Required fields are marked *

SHIRIKI KUONGEZA MISTARI