MISTARI YA WIMBO HUU

Ninaandika
Sababu nina vitu vya kuandika
Ninachana
Sababu nina uwezo usiofichika
Hii ni nje ya mtaala ndani ya ukweli
Nje ya masihara tofauti na kejeli
Kesho nikizikwa huu ni wosia
Kwa wale maskini ninaowapigania
Nikiwemo mimi na mamia kwa mamia
Lazima waelewe hamna haki Tanzania
Haki ya kuishi wala kutoa maoni
Nawekwa hatiani kwa kosa la mtu fulani
Au nasingiziwa ili niende gerezani
Hukumbuki Papii mwanangu Pinogora
Leo yuko wapi hakubali maisha bora
Kama haki mbinguni sheria duniani
Haki ya uraia haki ya elimu
Haki ya usalama kesho nisilaumu

Haki yangu iko wapi
Unaponidhulumu
Unaponihukumu bila kuwa na kosa
Haki yangu iko wapi
Ukishanimwaga damu
Ukishanifunga jela bila kuwa na kosa

Haki yangu iko wapi
Unaponidhulumu
unaponihukumu bila kuwa na kosa
Haki yangu iko wapi
Ukishanimwaga damu
Ukishanifunga jela bila kuwa na kosa

Mnyonge ameshanyongwa haki yake hajapatiwa
Sisi tabaka la chini kwa nini tunaonewa
Kwa wenye nazo haki inanunuliwa
Haya mambo ni ya kweli siyo ya kusimuliwa
Pita hospitalini mahakamani
Adui wa haki kashika usukani
Huduma haupati mpaka utoe chochote kitu mfukoni
Ndani ya nchi yangu mzalendo nalilia haki yangu
Kwa nini niipate kwa shida
Unayenibania unapata ipi faida
Ninachostahili nikipate kwa wakati NI HAKI
Sio mpaka nitoe noti SITAKI
Mlio kwenye vitengo msitese raia
Vaa viatu vyake muone anavyoumia
Nchi hii ni ya kwetu tuwe wazalendo
Tuongeze na upendo tuzidi kaza mwendo

Haki yangu iko wapi
Unaponidhulumu
unaponihukumu bila kuwa na kosa
Haki yangu iko wapi
Ukishanimwaga damu
Ukishanifunga jela bila kuwa na kosa

Haki yangu iko wapi
Unaponidhulumu
Unaponihukumu bila kuwa na kosa
Haki yangu iko wapi
Ukishanimwaga damu
Ukishanifunga jela bila kuwa na kosa

Watakaozikwa kwa msimamo MaKaNTa nasi tumo
Napata huu msukumo kupingana na huu mfumo
Jukumu kuwatoa watu wangu utumwani
Haki yangu duniani siridhiki magirini
Walileta dini tujizike maskini
Kwa hisani ya Marekani hayaishi mabalaa
Jaribu sema ukweli uone wanavyokukataa
Eti pesa inaongea ubinafsi unatugharimu
Akili zetu finyu hatusikii ya Mwalimu
Watu wangu wanakesha kwa kuomba miujiza
Wamekosa tumaini mfumo unawakandamiza
Wanawaza mbinguni hadithi za kusadikika
Nabisha kihuni hata hapa kitaeleweka
Wajue hali halisi hata wasio wadadisi
Huku mtaani ibilisi mawazo ni ya visasi
Silaha zinaelekezwa mahakamani na polisi
(Mahakamani na Polisi)
Yeah
Nataka haki

Toa Maoni Hapa

SHIRIKISHA MWINGINE

Your email address will not be published. Required fields are marked *

SHIRIKI KUONGEZA MISTARI