MISTARI YA WIMBO HUU

Tunda hali yangu mbaya
Ni bora mmekuja kuniona
Mnipe maneno ya mwisho
Kwani sina uhakika kupona
Mi sijapima ila na ngoma
Kwani dalili zote mi naziona

Hiyo sio ngoma labda ni homa
Usijali kachaa wangu utapona

Chege usinipe moyo
Usinipe moyo mi wa leo au wa kesho
Ona feni limewashwa lakini mwili unatoka jasho

Usikonde mwili kutoka jasho
Tunda
Mwili kutoka jasho
Tunda
Mwili kutoka jasho hali ya hewa mbaya
Usikonde mwili kutoka jasho
Tunda
Kutoka jasho
Tunda
Mwili kutoka jasho hali ya hewa mbaya

Eti kusikia baridi huku natoka jasho
Hiyo ni dalili ya nini niambie
Nahisi Iziraeli yuko hapa
Anasubiri anichukue

Hali ya hewa yaweza change
Bongo kila siku joto
Shika lesso futa jasho acha mawazo ya kitoto
Haujifahamu Tunda we ni binadamu
Embu inuka kwanza
Inuka twende tukapime damu

Nasema siendi kupima siendi
Nishakataa katukatu (kwanini Kwanini huendi)
Tunda naumwa sana nipo kwenye kitanda
Nasubiri mi kufa tu (amka bwana)
Nasema siendi kupima siendi
Nishakataa katukatu (kwanini)
Tunda naumwa sana nipo kwenye kitanda
Nasubiri mi kufa tu (okay)

Tunda hali yangu mbaya
Ni bora mmekuja kuniona
Mnipe maneno ya mwisho
Kwani sina uhakika kupona
Mi sijapima ila na ngoma
Kwani dalili zote mi naziona

Hiyo sio ngoma labda ni homa
Usijali kachaa wangu utapona

Okay
Nahisi uoga umetawala kwenye fikra za uso wako
Malaika wa msafara wanaulinda uhai wako
Usogope mgonjwa haupo peke yako
Embu lala kwanza
Lala uiboreshe afya yako

Naogopa hata kulala nahisi ntapitiliza
Sitoamka tena
Pole sana mwanangu Ramadhani
Baba ako hutoniona tena

Okay
Mbona Banza aliumwa lakini akapona
Akili inavonituma nisije kukuona
Poza na huna huruma kwanini hujapima
Tunda una moyo wa chuma kushinda hata Segea Juma

Pindi nikifumba macho nawaona kwa mbali
Malaika wananiita (acha uoga bana)
Hasira inajenga picha niko kwenye jeneza
Tayari kwenda kuzikwa
Hii dunia ni njia usia nawaachia
Jaribuni kuzingatia
Mapema mrudi kwa Mungu tena kwa haraka sana
Muanze kumsujudia

Tunda hali yangu mbaya
Ni bora mmekuja kuniona
Mnipe maneno ya mwisho
Kwani sina uhakika kupona
Mi sijapima ila na ngoma
Kwani dalili zote mi naziona

Hiyo sio ngoma labda ni homa
Usijali kachaa wangu utapona

Pole bana
Pole sana (pole sana)
Pole bana (kwanza ni lazima upime)
(Ujue unaumwa nini sio unanung’unika tu)
(Au sio Tunda eh)
Pole sana (pole pole)
Pole bana (pole Tunda)
Pole

Toa Maoni Hapa

SHIRIKISHA MWINGINE

Your email address will not be published. Required fields are marked *

SHIRIKI KUONGEZA MISTARI

VIDEO YA WIMBO HUU