MISTARI YA WIMBO HUU

Ilikuwa ni siku ya furaha
Vifijo nderemo na shamra shamra
Uliponivika pete kidoleni mwangu
Kwa sura ya furaha tabasamu thabiti
Ukatamka maneno matamu moyoni mwangu
Mbele ya wazazi wako wazazi wangu
Na zaidi mbele ya Mungu wako
Sasa kwanini leo wataka rudi nyumbani kwenu
Mambo madogo dogo haya yasikukasirishe mamii

Hasira hasara
Mami wangu
Hasira hasara
Hasira mbaya mama
Hasira hasara
Mami wangu wa maisha
Hasira hasara
Acha hiyo kabisa
Hasira hasara
Huku nyumbani tena
Hasira hasara
Watoto wa nani hawa
Hasira hasara
Rudi tena kwa mara ya pili
Hasira hasara

Ninachokumbuka nilikueleza
Kabla hujakubali
Kubwaga manyanga na kukubali kuwa mwili moja nami
Ili tuelewane tusije kwazana mami wangu
Lakini ni kitu kidogo tu kinakuboa
Kitu kidogo tu kinakuudhi
Kitu kidogo tu wataka kwenda nyumbani
Mami acha hizo ah
Mami acha hizo

Hasira hasara
Hasira hasara
Hasira hasara
Mami elewa hilo
Hasira hasara
Mungu wangu hapendi
Hasira hasara
Kusamehe unakufa
Hasira hasara
Nisamehe mama
Hasira hasara
Hasira hasara
Moyo unahangaika balaa
Hasira hasara
Hasira hasara aah
Hasira hasara aah

Nieleze nijue hasira ya nini
Nieleze ili nitambue kosa langu mama
Nieleze nijue hasira ya nini
Nieleze ili nitambue kosa langu mama
Kosa langu mama lipo wapi mama

Hasira hasara
Yei yei yeeh
Hasira hasara
Makosa yapo
Hasira hasara
Yanapaswa samehewa
Hasira hasara
Najua nimekosa
Hasira hasara
Naomba msamaha
Hasira hasara
Naomba rudi tena
Hasira hasara
Turudishe ukurasa upya
Hasira hasara
Kumbuka ahadi yako

Watoto wanahangaika wewe haupo
Tuliwaleta wote tuwatunze wote mpaka mwisho mama
Hasira hasara hasira hasara
Hasira hasara mami rudi aah
Hasira hasara

Hasira hasara
Wou wou woo
Hasira hasara
Nisikilizeni wote
Hasira hasara
Mnaoishi kwenye ndoa
Hasira hasara
Hasira inaua
Hasira hasara
Mahusiano ya wawili
Hasira hasara
Utauza hadi nyumba
Hasira hasara
Kwa ajili ya hasira
Hasira hasara
Hasira iondoeni
Mkuze pendo lenu ba
Kwa wote aah
Hasira hasara
Hasira hasara

Toa Maoni Hapa

SHIRIKISHA MWINGINE

Your email address will not be published. Required fields are marked *

SHIRIKI KUONGEZA MISTARI

VIDEO YA WIMBO HUU