MISTARI YA WIMBO HUU

Hawajui tulipotoka, watatuacha tunapokwenda
Ya kwao yanawashinda, yetu hawataweza
Hawajui tulipotoka, watatuacha tunapokwenda
Ya kwao yanawashinda, yetu hawataweza

Suruali zinanifunguka vicheche vikikatisha
Mshahara ukitoka sirudi mpaka umekwisha
Nikirudi nane usiku, nalala na viatu
Chicha chakari sikumbuki hata ndoa yetu
Nikiwa na wewe moyoni napata aibu
Ukisoma macho utajua navyokugiribu
Sikawii kuharibu, nakosa sana adabu
Nakushangaa mwanamke una moyo wa ajabu

Siwezi kukuacha laazizi
Mwenyewe siwezi ishi
Tuliumbwa wote mpenzi
Wewe uishi na mimi

Umefunzwa utotoni, umefundwa unyagoni
Kulea mwanaume lakini sio kama mimi
Usiku uliopita nimekupa ngeo mdomoni
Asubuhi ulipoamka ukasema umeniota mimi
Una mapenzi hata shetani angeyaogopa
Sirudishi hata robo ya unavyonipa
Hata washikaji zangu wanakiri kuwa sikufai
Kama ni adhabu nastahili nizikwe hai, yeah!

Hawajui tulipotoka, watatuacha tunapokwenda
Ya kwao yanawashinda, yetu hawataweza
Hawajui tulipotoka, watatuacha tunapokwenda
Ya kwao yanawashinda, yetu hawataweza

Amani bila silaha, niache tu niende laazizi
Usione huruma bado siyawezi mapenzi
Mi kicheche huniwezi usiogope kuniacha mpenzi
(Kukosea ni ubinadamu wakuvu kuithamani hiyo)
Watoto wa nje kibao, tena wasio na malezi
Na matusi ya mama zao yote huja kwako mpenzi
Nini unanipendea? Mwanaume na sifa mbaya!
Rafiki zako wote wananiita malaya
Napenda uwe na mume, lakini sio mimi
Sitaki tuachane nakuomba uniache mimi
Hustahili uchezewe, sistahili kuwa na wewe
Umefanana na utulivu uwekwe ndani uolewe

Waweza kuta firauni peponi
Taulo langu niendapo bafuni
Nauli yangu niwapo safarini
Usiende mbali na mimi

Kwangu u malkia
Kwa vile cheo kingine chochote hakitakufaa
Naamini utanisikia kwa vile unanizimia
Hata upewe dunia hautakaa kunirudia

Hawajui tulipotoka, watatuacha tunapokwenda
Ya kwao yanawashinda, yetu hawatoweza
Hawajui tulipotoka, watatuacha tunapokwenda
Ya kwao yanawashinda, yetu hawatoweza

Hawajui tulipotoka, watatuacha tunapokwenda
Ya kwao yanawashinda, yetu hawatoweza
Hawajui tulipotoka, watatuacha tunapokwenda
Ya kwao yanawashinda, yetu hawatoweza

Jay Dee na Binamu pamoja twawakilisha oh
(Binti machozi iyee!
Na Binamu 13, toka E-Jeez
(Complex, I see you boy!)

Toa Maoni Hapa

SHIRIKISHA MWINGINE

Your email address will not be published. Required fields are marked *

SHIRIKI KUONGEZA MISTARI