MISTARI YA WIMBO HUU

Yeah (let’s go)
Yes
Unga waya kwenye spika
Kisha weka fire kwenye reefa
Mtaftie malaya senorita
Mguu mdogo ntakupwaya kama sniker
Nafuu mgogo kuliko wahaya wanavyosifika
Twende sawa mi ni dawa kwenye fever
Home sio Kipawa Popo Bawa wala Sinza
Kama kawa ukipagawa nakuliza
Wazawa nawapaisha mpaka ulaya kama visa
Weka umakini kando ukose bundle za ku-surf
Dili na mgambo ili akuvunje ka bango chafu
Mi ni staa wa Billboard na msomi mwanafalsafa
Naslaa kama Wilbrod hamuoni bado mna suffer
Hii ni original ndo maana ina-sound kama demu
Enzi hizo game haiko virgino underground walikuwemo
Pure facts ndani ya pure maths
Ukimtoa Duke maproducer wengi wa Bongo pre-mature cats
Mitaani sionekani kama jini
Dada ‘ako anatamani kuwa na bwana kama mimi
Mashetani yanagani kwa imani kama dini
Zao jipya hewani pole zama za tisini
Na-pimp big kwa hisia ka Ben Carson
I think big naingia ubia na main persons
Kama rap ni soka mi ni footballer
The hood baller haina ku-beep na full dollar
Don katage na jambazi nabless pistu
Ibilisi huna chako ume-mess na Yesu Kristu
Nasema ukweli ambao matozi wanauficha
Ubabeli ndo umefanya mifeli words and pictures

Akili zangu sio fyatu nikisema watu sio wema
Kilema katoa taki na upendo sio upendo tena
Nimeona mapema hawapendi kuona unahema
Labda unachechema hauwezi unatema
Ukirusha unadema
Mipango hiyo inabuma kisa jirani
Unafichwa gizani wapo ‘api ukipita mibani
Ukikatiza nyikani na wakufute kwenye ramani
Pesa ikukimbie kifupi ufulie ka zamani
Muumba akuchukie tena akunyime thawabu
Dhambi zao ulipie mambo yakupindie bila sababu
Kote wasimulie upigwe majungu ka Taarabu
Haina ustaarabu bila kosa wakushikishe adabu
Yoh unakesha unawaza haupati majibu
Unaamua kukaza na bado magumu yanasibu
Unachanganya ladha tofauti za pombe balaa
Usipagawe brother jikaze ndo ilivyo mitaa
Yupi utamuamini wengi mapitini ma-snitch
Wapige chini treni itarudi relini sikufichi
Haina kufichana kujuta kushika tama
Sio juzi na jana watu hawaaminiki toka zama
Kichwani una mawazo demu wako kashakutosa
Fedha hauna yule anazo aki-beep anatuma vocha
Kata pochi upate penzi hauna guu la chochoro
Ushafanyiwa ushenzi kila unaporudi mgogoro
Pigana na hela kisela maneno sio bunduki
Ukisema ulazwe Mwaisela songa mbele kichwa mkuki
Toka nduki
Tusi watupie chuki wachukie
Tena usiwanunie sana ujutie wakahadithie

Nachokumbuka alimuamini kama mchungaji wa kanisa
Yote yanayosemwa mtaani hakujua kama yanamgusa
Akaona bora afeli shule mwisho akafaulu mapenzi
Mashauzi ndo vile mwishoni yamekuwa majonzi
Hakujua yesu wa mapenzi mitaani watu wangemuita
Aliemuamini kama mpenzi kawa Yuda leo yamemkuta
Drop love kwenye usasa so long ka bi Kidude
Unampenda kisha unamuacha asikutapeli kama Dude
Leo anataka second chance ka Salvado Solenza
Alishacheza first chance ka movie cheki anakonda
Rahisi sana kukubali kile ambacho ye anajua
Hata kama atakuja feli kwa vitendo sio kuongea
Anakumbuka game tough ye na mpenzi walizocheza
Leo ana-drop kama Klof uchaguzi daily wanammeza
Kila anaesoma likizo sio kweli kwamba ana supp
Watoto wanawapita kiuwezo watu wazima mpaka wana-stop
Ah we utaona ndo unapendwa kumbe ndo unachunwa
We unaona ndo unapanda kumbe ndo unavunwa
Ushambandika kama sticker ukimbandua ndo unasepa
Usije ukatekeka akakumwaga ka ana tipa
Ah nilipendwa mpaka wapangaji nyumbani wakawa wananuna
Leo love imegeuka mtaji kwenye mzani watu wanapima
(sio siri haya mambo) nishayaona kijana
Demu flani kamteka mwana mpaka mia anabana
Washatumia sana pesa hafu wakaja wakaachana
Demu kaongwa mpaka Chaser kumbe kuna boya anambana
Sio kila anaebeba begi ukadhani shule anaelewa

Hii ni siri yenye laana kama tupu ya mzazi
Kwa roho mkunjufu sitoruhusu utundu wazi
Sizungumzi na mwana nazungumza na mzazi
Huu uzungu wa kuuzana kama ruzuku ya jambazi
Kumbuka wema watoto waukwepe mkosi
Baba ana nyumba ndogo kigezo kubwa haitoshi
Anazuga anakupa support Yuda Eskarioti
Pochi inashinda kwa mchumba bi mkubwa ale karoti
Ona kijana amekosa malezi kisa
Mama hana uwezo baba yupo kwa mpenzi Lissa
Ama baba hana uwezo na mama haiwezi shida
Enzi zimepita kisa ana mpenzi wa kumridhisha
Kumbuka haya maisha safari
Pole kwetu walokufa wamemaliza tayari
Wasifu wa sifa sio sifa jijali
Njoo pata maarifa hii taarifa ya habari
Ona watoto wanaomba wanakosa na wana njaa
Kwa sababu wazazi waliponzwa na tamaa
Hili janga la jamii sio janga la jamaa
Binti mwenye kilanga kalamba dume la mtaa
Hii ni kwako wewe rafiki yako jihami
Kama huna nia njema huwezi kuwa jirani
Sina imani nawe usiwe na imani nami
Kama sote si wanyama mi ni simba we ni nyani
Ila usilie mama kaza moyo we shujaa
Ingawa dhiki iko uraiani na imani imeshiba njaa
Kuwa na imani ili amani ipate nafasi
Mchunge mwana wa jirani asidanganywe na fataki

Toa Maoni Hapa

SHIRIKISHA MWINGINE

Your email address will not be published. Required fields are marked *

SHIRIKI KUONGEZA MISTARI