MISTARI YA WIMBO HUU

Nawajuwa wadada kabla sijabalehe
Miaka kama saba mitaani nasujudiwa
Nilikuwa mafia, ninja, usiombe
Nkukute na mazaga yote lazima nikombe
Nakupa zuna, mawashi, mateke
Teja akileta simu namgalila ka kete
Nshauza poda but sijawahi kumoka
Nshauza ganja ila sijawahi kunyonga
Nilikuwa mnoma toka wakati nasoma
Walimu walinikoma napogoma kusoma
Niliacha shule toka darasa la tano
Usicheze na elimu, embu fata hii mifano
Natega shule nakwenda kubana kete
Home wakizingua naona bora nisepe
Nilivunjwa miguu na polisi wa Kisutu
Nilikwenda kuvunja kwenyee duka la ujugu
Yoh, my mama alilia sana
Mkononi nina pingu nimelazwa Amana
Yoh, kwa nguvu za Maulana
Baada ya miezi mitatu nikaweza kusimama

Majuto ni mjukuu
Yashanikuta makuu zaidi ya moto wa kifuu
(Sikiliza hii story eh)
Niliyofanya ni kufuru
Nahitaji kuiona nuru, ili nami niwe huru
(Diss na hii story eh)
Humu ndani sina raha
Kila siku ni balaa, watu tunalala njaa
(Sikiliza hii story eh)
Kazi ngumu kila saa
Ole wako ukikataa, utakufa huku umekaa

Yoh, 99 ndo nilifanya kufuru
Nikaharibu home ili niende kwa Kaburu
Nikapita border Tunduma mpaka Lusaka
Bahati mbaya mamwela wakaninyaka
Nikarudishwa Dar, bongo.com
Home nilizingua bora nika-chill Dom
Kuna wanangu wabishi yaani usiombe
Usiku wa manane dili zetu kuiba ng’ombe
Hawa wana ni maku, malizia na ma
Bado tuibe mmoja wao wanaleta tamaa
Masai akatokea ikawa vita ya visu
Issa Mbebe aka-dead, rest in peace and I miss you
Nkaona dah! Bora nirudi Dar
Mpaka leo nahema cause nilisikia pah!
Nikiwa ndani ya basi na mawazo msururu
Kuvunja, kuua na kumbaka Nuru
Na story mbaya imeganda ubongoni
Nshapigwa na visu na machizi Kinondoni
Ile kushuka Ubungo tu wazee hao hapa
Ndo maana mpaka leo wakiri unaniona hapa

Majuto ni mjukuu
Yashanikuta makuu zaidi ya moto wa kifuu
(Sikiliza hii story eh)
Niliyofanya ni kufuru
Nahitaji kuiona nuru, ili nami niwe huru
(Diss na hii story eh)
Humu ndani sina raha
Kila siku ni balaa, watu tunalala njaa
(Sikiliza hii story eh)
Kazi ngumu kila saa
Ole wako ukikataa, utakufa huku umekaa

My mama alilia sana
Mkononi nina pingu nimelazwa Amana
Yoh, kwa nguvu za Maulana
Baada ya miezi mitatu nikaweza kusimama
(Sikiliza hii story eh)
(Diss na hii story eh)
(Sikiliza hii story eh, oh)

Majuto ni mjukuu
Yashanikuta makuu zaidi ya moto wa kifuu
Niliyofanya ni kufuru
Nahitaji kuiona nuru, ili nami niwe huru
Humu ndani sina raha
Kila siku ni balaa, watu tunalala njaa
(Sikiliza hii story eh, ooh)

Toa Maoni Hapa

SHIRIKISHA MWINGINE

Your email address will not be published. Required fields are marked *

SHIRIKI KUONGEZA MISTARI