MISTARI YA WIMBO HUU

Yeah
Hii ni habari njema
Hii ni moja ya ngoma inayowakilisha vyema
Hisia za mtu aliyetemwa
Naheshimu tabia nyingi za vijana
Ila sio za kuziendekeza sana
Kama kupenda ni mtihani wa kila kijana
Kaza

Na mawazo kichwani uko wapi hivi kwani
Navyoku-miss hadi nalia naishia kukuona pichani
Uzuri wako umeni-cost mi dai sio ka dukani
Ukiniona nime-lost nishakosa ramani
Napenda kujizuia nisiwe hata nakuwaza
Niliyempenda amekimbia sijui nlishindwa kumkataza
Nimebaki naugulia sina hata wa kuniliwaza
Ka sipo ndani ya dunia kote kumenyamaza
Sa nimepata mwenye figure ila huyu anaringa
Anaringa on every finger
Walompa washaanza kuniwinda
Dah ulikuwa ukitabasamu sio tu kwenye good times
Umeniacha nina hamu baada ya kunionjesha utamu
Na nahisi hiyo figure ulionekana hata umekaa
Ba-basi nilifika ila nikakosa pakukaa
Roho inahuzunika na furaha imekwisha

Nikisema niko busy hujali
Nsipopiga simu usiku hujali
Nkikwambia sina kitu unasema nsijali
Nkafurahi kila siku nlihisi nimepata zali
Nikisema niko busy hujali
Nsipopiga simu usiku hujali
Nkikwambia sina kitu unasema nsijali
Ila hatari mwisho wa siku umekwenda mbali

Maji ya moto kwa baridi ina maana hamna joto
Hata mtoto kwa mkaidi si kwamba hamna mboko
Kukupenda nilijitahidi ila umeniacha kwenye chocho
Sijui akili ulinizidi au ndo hivyo niko soso
Si wakati tunapendana haya tulishayaongea
Ikawa tuombe kwa Maulana tu yasije kutokea
Leo wapi ulipoelekea hadi usahau ulipotokea
Nakupenda honey nateswa na haya mazoea
Mapenzi mnapopendana ushenzi mnapotengana
Kuwa crazy inawezekana kwa wezi walivyojazana
Umeniacha sina amani wala raha niko ndani
Niende studio nampigia Mbezi wapi hapatikani
Huenda mi nilikupenda ila we ulinitamani
Kweli umenipenda ila unapoenda ni gizani
Unafeli (mama) au umepandwa na shetani
Kweli siko sawa Nambie nakosa gani

Nikisema niko busy hujali
Nsipopiga simu usiku hujali
Nkikwambia sina kitu unasema nsijali
Nkafurahi kila siku nlihisi nimepata zali
Nikisema niko busy hujali
Nsipopiga simu usiku hujali
Nkikwambia sina kitu unasema nsijali
Ila hatari mwisho wa siku umekwenda mbali

Mapenzi yangu gado
Kuchoshwa na mpenzi wangu bado
Ah ila mwenzangu hufagilii
Navuta waya natupa text hufatilii
Ah basi mi yangu macho
Na nitafutwa na ndugu zangu jasho
Ah napigwa jiwe na Young Dee
Kwa sababu ya mapenzi crazy baby

Nikisema niko busy hujali
Nsipopiga simu usiku hujali
Nkikwambia sina kitu unasema nsijali
Nkafurahi kila siku nlihisi nimepata zali
Nikisema niko busy hujali
Nsipopiga simu usiku hujali
Nkikwambia sina kitu unasema nsijali
Ila hatari mwisho wa siku umekwenda mbali

Nimenasa mpenzi umenikimbia
Umeniacha kipenzi wapi ntakimbilia
Nimedata kishenzi ah ka umeshtukia
Maana sitaki kufikiri ulikuwa ukiniibia
Nimenasa mpenzi umenikimbia
Umeniacha kipenzi wapi ntakimbilia
Nimedata kishenzi ah ka umeshtukia
Maana sitaki kufikiri ulikuwa ukiniibia

Toa Maoni Hapa

SHIRIKISHA MWINGINE

Your email address will not be published. Required fields are marked *

SHIRIKI KUONGEZA MISTARI