MISTARI YA WIMBO HUU

I don’t wanna be so lone
I don’t wanna walk alone
I don’t wanna stand alone
I don’t wanna be alone
In the world

Wanadamu huwa wepesi kudharau
Misukosuko ikipungua basi na Mungu ndo wanamsahau
Wengine amani inatoweka hawakumbuki walikotoka
(Success) wazipatazo wao wanaona ka wameokota
Siku bado zinapita na mengi yanabadilika
Umri unaongezeka mambo mengi umeshapitia
Ila nakuona mnyonge na umekata tamaa
Basi piga moyo konde na uzidi komaa (komaa)
Safari uliyokuwa nayo hapa duniani
Safiri kwa imani kwani ujue siku hazifanani
Kwani naamini hakuna anaejua mbele sidhani
Zaidi ya Maanani ambaye ndio nguzo hapa duniani
Shukuru kwa kila jambo liwe baya au jema
Ndo mapenzi yake tu so niamini nachosema
Muache aitawale aiongoze roho yako
Ujifungue kwenye pingu za maovu uwe peke yako

I don’t wanna be so lone
I don’t wanna walk alone
I don’t wanna stand alone
I don’t wanna be alone
In the world
I don’t wanna be so lone
I don’t wanna walk alone
I don’t wanna stand alone
I don’t wanna be alone
In the world

Magari ya kifahari
Nyumba za ghorofa shilingi na dollar
Unatawala umesoma sana
Mambo haya ya dunia tafadhali sikiliza
Maisha ni moja kifo ni siku moja
Shida ni kuingoja piga magoti wewe omba

I don’t wanna be so lone
I don’t wanna walk alone
I don’t wanna stand alone
I don’t wanna be alone
In the world
I don’t wanna be so lone
I don’t wanna walk alone
I don’t wanna stand alone
I don’t wanna be alone
In the world

Kitu bora kuhusu kesho ni uwe bora zaid ya leo
Maisha matokeo na Mungu ndo letu kimbilio
Aliyekuvusha kwa milima atakuvusha kwa mabonde
Basi usitazame nyumba zidi songa mbele twende
Pumzi kakupa nani Shukuru utapungua nini
Vyote kakupa yeye na bado humthamini
Vito pesa na mali zenye thamani
Zisikufanye udiriki ukapungukiwa na imani
Kumsahau kumdharau kutomwamini aleyekupa
Kujiona juu umepanda dau na kujikuta umeanguka
Basi muombe akusamehe maisha yako akuendeshee
Mabaya yote akuepushe uishi raha mustarehe
Sema ‘asante Mungu’ kwa kila siku unayoanza
Na pia ‘asante Mungu’ kwa kila siku unayoenda
Mungu wa watu weupe ndio Mungu wa watu weusi
Usimkumbuke tu wakati wa matatizo change upesi

I don’t wanna be so lone
I don’t wanna walk alone
I don’t wanna stand alone
I don’t wanna be alone
In the world
I don’t wanna be so lone
I don’t wanna walk alone
I don’t wanna stand alone
I don’t wanna be alone
In the world

Sio kila siku tunaongelea mapenzi
Sio kila siku tunaongelea anasa na mambo ya kidunia sometimes
Tukumbushane kumuomba yule aliyetuwezesha kuwa hapa duniani
Yule aliyetuwezesha kuusikia na kuuona wimbo huu
Mungu ni mmoja amini hivyo
Ndio kimbilio la mwisho na nguzo yako hapa
Na baada ya kutoka hapa duniani
Mungu wa matajiri ndio Mungu huyo huyo wa masikini
Kwahiyo kila mmoja ana azima yake kwake
Basi tusimsahau tuwe karibu yake
Na tumshukuru kwa kila jambo
Kila mmoja ana azima yake kwake
Basi tusimsahau

Toa Maoni Hapa

SHIRIKISHA MWINGINE

Your email address will not be published. Required fields are marked *

SHIRIKI KUONGEZA MISTARI

VIDEO YA WIMBO HUU