MISTARI YA WIMBO HUU

Matapishi ni kinyaa
Kuzirudisha tena kwenye kinywa
Japo mengi ulisema
Kama nuru ghafla ukazima
Ikawa ngumu kukusahau
Nikasema moyo ukome
Kwa kali sulu na madharau
Penzi ulivunja na ngome

Na unajua hata nikilia
Siwezi kutokwa na machozi
We ndo ulifanya macho yangu
Nione wengi waongo
Aa ukaudhurumu moyo wangu
Uliuza penzi kwa magendo
Leo unatamani wewe kurudia zamani
Ni ndoto
Wewe nirubuni kwa penzi la kidani
Kama mtoto

Mi na wewe
Acha ibaki stori mi na we
Mapenzi mi na wewe
Acha ibaki stori mi na wewe
Mi na wewe
Acha ibaki stori mi na we
Mapenzi mi na wewe
Acha ibaki stori mi na wewe

Kiliniumiza kitanda
Na shuka tuliolalia
Mapenzi yana siri kubwa
Sishangai mtu akilia
Nimekubali mboni zangu
Zimtazame mwingine
Maridhia ya moyo wangu
Huenda si fungu pengine
Cha kushangaza hadharani
Mengi ya kuficha ukaweka wazi
Nikahisi sijui mapenzi
Labda kwako sinogi nazi

Na unajua hata nikilia
Siwezi kutokwa na machozi
We ndo ulifanya macho yangu
Nione wengi waongo
Aa ukaudhurumu moyo wangu
Uliuza penzi kwa magendo
Leo unatamani wewe kurudia zamani
Ni ndoto
Wewe nirubuni kwa penzi la kidani
Kama mtoto

Mi na wewe
Acha ibaki stori mi na we
Mapenzi mi na wewe
Acha ibaki stori mi na wewe
Mi na wewe
Acha ibaki stori mi na we
Mapenzi mi na wewe
Acha ibaki stori mi na wewe

Yalinitesa mazoea haya
Lakini mi nishazoea mwaya
Ila tambua mapenzi mabaya
Kidonda chake hakinaga dawa
Ee mazoea aah
Lakini mi nishazoea mwaya
Ila tambua mapenzi mabaya
Kidonda chake hakinaga dawa

Mi na wewe
Acha ibaki stori mi na we
Mapenzi mi na wewe
Acha ibaki stori mi na wewe
Mi na wewe
Acha ibaki stori mi na we
Mapenzi mi na wewe
Acha ibaki stori mi na wewe

Toa Maoni Hapa

SHIRIKISHA MWINGINE

Your email address will not be published. Required fields are marked *

SHIRIKI KUONGEZA MISTARI