MISTARI YA WIMBO HUU

Ah yeah
Sipo kama nilivyokuwa haimaanishi niko tofauti
Iwe kiroho kimwili kiakili mashairi na hii sauti
Mi nacheni emcee shupavu mwenye verse hadimu
Asiwe hygenic ni ile chicken life left in him
Sista duu ukiibiwa moyo usilie mfanye awe official
Kidume atulie umuibie jina la mwisho
It’s giving checking this world
Kuna friends na foes
Kuna snake fake niggas na ma-jiggerlo
Ukiwa wa ukweli hau-bounce na hautofeli
Ubingwa unashika fasta ka mimba na mahausigeli
Wananiita mamlaka ya reli kwa hii train on thoughts
Ni kawe rebirth ya Makaveli brain drain niondoke
Haikiwi effective bila juhudi nisichokiamini haki-happen
Naeza lala na bundi na ukaamka mwenye bahati
Usilale fofofo ruzuku itakwisha
Utatembea hovyo ka kuku aliyekatwa kichwa
Maisha yako fast na yana speed ya light
Unaeza freeze kama ice ndani ya fridge ya Sykes
Ukienda mbio na muda mtapishana
Mafanikio huja kwa kupenda unachokifanya

Ielewe mitaa kisha ielewe sanaa
Nawapita mmekaa natisha jamaa
Ukibisha ntakushangaa
Kufundisha mi nafaa
Nalisha wenye njaa naweza rudisha masaa
Ielewe mitaa (ielewe ikuelewe)
Ielewe sanaa
Nawapita mmekaa natisha jamaa
Ukibisha ntakushangaa
Kufundisha mi nafaa
Nalisha wenye njaa
Naweza rudisha masaa ielewe mitaa

Usiache ulichotaka maishani ghafla tu na kufuata kile ulichotamani
Ielewe ikuelewe kama oxygen na carbon
Hauwezi game bila pain muulize Saigon
Naishi kiboss na usanii haupotei
Natumia noti tangu ina sahihi ya Mtei
Niletee mabumunda mjeshi nikiwa vitani
Nikikuta mnaabudu punda ntawapelekea majani
Wangapi huji-stress hujitia mapozi na hawajielewi
I’m such a nut case naeza nka-divorce ya hail Mary
Funny huh sijui serious yuko wapi
I make cred goes in the front row forward laughing
Ni ngumu kuitafuna usiimeze haraka
Sumu ushakunywa jiandae tu kucheza salsa
Urembo na uzuri upo ndani kwa nje mnajiongopea
Muuza sura usikose amani makunyanzi yakikutokea
Badili mwendo mkwepe skendo mwache aende zake
Au muonyeshe upendo tembo hachoshwi na pembe zake
Ujinga ni mjukuu wa uoga yule aliyemzaa chuki
Vina vinanipa nyota unaonifaa kama mkuki
Simmwagii chumvi konokono asiye na gamba
Na simkumbatii nyuki kwa maono ya asali kuilamba
Ielewe ili usionewe usinyonywe usipuuzwe tena
Unyonge uondolewe usonge mbele wewe uishi vyema

Ielewe mitaa kisha ielewe sanaa
Napita mmekaa natisha jamaa
Ukibisha ntakushangaa
Kukufundisha mi nafaa
Nalisha wenye njaa
Naweza rudisha masaa
Ielewe mitaa (ielewe ikuelewe)
Ielewe sanaa
Napita mmekaa natisha jamaa
Ukibisha ntakushangaa
Kukufundisha mi nafaa
Nalisha wenye njaa
Naweza rudisha masaa ielewe mitaa

Ielewe ikuelewe

Toa Maoni Hapa

SHIRIKISHA MWINGINE

Your email address will not be published. Required fields are marked *

SHIRIKI KUONGEZA MISTARI

VIDEO YA WIMBO HUU