MISTARI YA WIMBO HUU

Ingekuwa vipi angekuwa hai D-Rob?
Na Chief Ramso angekuwa Bongo?
Wahisani bila kidato, na umrudishe K-Single?
Kwanza ingekuwa mfano, wao tayari ingekuwa chongo
Kati ya nani angekuwa wigo, na nani angekuwa mzigo

Ingekuwa vipi Balozi na Mr II (Mr II)
Wafanye vita ulingoni usiseme su (usiseme su)
Unajua nani kati angeibuka mikono juu?
Sema nani kati angeibuka mikono juu

Ingekuwa vipi Dully Sykes angeimba hardcore?
Mashairi kama Jay Moe, neno “wanasesere” naimani lisingekuwapo

Mauzo ya Rap ya Bongo yangefika platinum tano
(Mauzo ya Rap ya Bongo yangefika platinum tano)

Ingekuwa vipi HBC bila Jay? (bila Jay)

Ingekuwa sawa na The Wailers bila Marley (bila Marley)

Hiyo ni sawa kuwepo Snoop bila Dre (bila Dre)
Makumbusho bila kijiji au Bongo bila Nyerere

Ingekuwa vipi maisha ya Temeke yangekuwa juu kidogo
Unadhani wasanii wangejiita Walume Ndago?

Ingekuwa vipi Bongo Record isingekuwa ya Khalfani?
Watu kama flani flani tusingewasikia hewani

Angeimba nini Sista P asingekuwap Zey B?

Na ingekuwa wapi RnB asingekuwapo Jay Dee?

Angeimba nini Sista P asingekuwap Zey B?

Na ingekuwa wapi RnB asingekuwapo Jay Dee?

Nawaza mambo kwa kina, na bado majibu sina
Uwezo wa Mungu unaonekana, angeamua ingewezekana

Nawaza mambo kwa kina, na bado majibu sina
Uwezo wa Mungu unaonekana, angeamua ingewezekana

Ingekuwa vipi? (ingekuwa vipi?)
Ingekuwa vipi? (ingekuwa vipi?)
Ingekuwa vipi? (ingekuwa vipi?)
Ingekuwa vipi? (ingekuwa vipi?)
Ingekuwa vipi? (ingekuwa vipi?)
Ingekuwa vipi? (ingekuwa vipi?)
Ingekuwa vipi? (ingekuwa vipi?)
Ingekuwa vipi? (ingekuwa vipi?)

Ingekuwa vipi Bongo mitumba isingehalalishwa?
Masista duu, pedopusha vipi wangeshonesha?

Vitovu wangetuonyesha, je mapozi yangekwisha?
Au pigo gani brazameni leo zingemdatisha?

Ingekuwa vipi Bongo wasingekuwapo changudoa?
Wateja wao je wangewaopoa makaka poa?

Au pengine matendo ya ubakaji yangewaingia
Au labda ni mastashefu ndio zingewaokoa

Ingekuwa vipi kasi ya ukimwi kusingekuwa condoms?
Yaani ingekuwaje bila ukimwi tungetinga condoms?
Au ukimwi ungekuwepo halafu hakuna condoms
Unadhani mi ningesema “mi na mabinti damdam”?

Ingekuwa vipi ulipe buku tu kwa kila pumzi?
Kiumbe gani angediriki leo kupiga mluzi?
Unadhani ni watu wangapi wangekuwa wazima?
Labda tajiri, mafukara si tusingepona

Ingekuwa vipi kama Bongo ingekuwa kama New York?
Washikaji wangejazana ubalozini kuomba visa?

Au visa tungezipata bila kuongea kingereza
Kama sio chizi hutawaza, maswali mi najiuliza ingekuwa vipi

Nawaza mambo kwa kina, na bado majibu sina
Uwezo wa Mungu unaonekana, angeamua ingewezekana

Nawaza mambo kwa kina, na bado majibu sina
Uwezo wa Mungu unaonekana, angeamua ingewezekana

Ingekuwa vipi? (ingekuwa vipi?)
Ingekuwa vipi? (ingekuwa vipi?)
Ingekuwa vipi? (ingekuwa vipi?)
Ingekuwa vipi? (ingekuwa vipi?)
Ingekuwa vipi? (ingekuwa vipi?)
Ingekuwa vipi? (ingekuwa vipi?)
Ingekuwa vipi? (ingekuwa vipi?)
Ingekuwa vipi? (ingekuwa vipi?)

Ingekuwa vipi Yesu angerudi
Angeimaliza vita wapalestina na wayahudi?
Fikiri ungeisha vipi mgogoro wa nchi ya ahadi
Na fikiri uwepo wake ungeokoa maisha ya wangapi?

Ingekuwa vipi kama Osama angeutawala ulimwengu?
Wamarekani uarabuni wangekuwa sungusungu?
Je magaidi wangekuwa nani, ma-black au wazungu?
Warabu wangeelimika, wangetoka kwenye ukungu?

Ingekuwa vipi ulimwengu kama kusingekuwa na dini?
Dunia bila dhambi, kipimo cha uovu nini?
Polisi, mahakama na gerezani angeenda nani?
Huhitaji idhini tathmini, ingekuwa vipi hali ya amani

Vipi kama duniani wangekuwa mabinti peke yao?
Je wangetembea uchi kwa sababu hakuna wenzao?
Au wangejisitiri, mitindo ingekuwa ya nini?
Ya kazi gani? Kama hakuna wanaume duniani

Vipi kama wazungu wasingeingia Afrika
Unadhani maendeleo kwetu yangechelewa kufika?

Magari, ndege, reli, nani angeleta?
Na bila ya biashara ya utumwa wangekuwepo black americans?

Nawaza mambo kwa kina, na bado majibu sina
Uwezo wa Mungu unaonekana, angeamua ingewezekana

Nawaza mambo kwa kina, na bado majibu sina
Uwezo wa Mungu unaonekana, angeamua ingewezekana

Ingekuwa vipi? (ingekuwa vipi?)
Ingekuwa vipi? (ingekuwa vipi?)
Ingekuwa vipi? (ingekuwa vipi?)
Ingekuwa vipi? (ingekuwa vipi?)
Ingekuwa vipi? (ingekuwa vipi?)
Ingekuwa vipi? (ingekuwa vipi?)
Ingekuwa vipi? (ingekuwa vipi?)
Ingekuwa vipi? (ingekuwa vipi?)

Toa Maoni Hapa

SHIRIKISHA MWINGINE

Your email address will not be published. Required fields are marked *

SHIRIKI KUONGEZA MISTARI