MISTARI YA WIMBO HUU

Huwezi kuwa sahihi wa kila jambo
Mi binadamu sijakamilika
Mengi yamenisibu kitambo
But leo yamenifika
Sina uhakika ntakuudhi au ntabaki happy
Au utaleta mashauzi au utachukulia kiroho safi
Ningeomba Mwenyezi anipe baraka hata tonye
Kabla sijatoka kimuziki nikatamani nikuone
Baraka zikafika juu nikakutana nawe
Instagram duh Nikabahatika ku-chat nawe
Kiuhakika ndoto yangu ya kwanza ikawa imetimia
Nikafarijika siku zikapita nikakazia
Kutafuta namba yako lakini sikuipata
Popote niendapo nikakosa mpaka ukapita mwaka
Kucheki Insta Message tukaanza ku-chat
Nikatuma message “Mambo?”
Ukanijibu “Safi”
Nikakuomba namba ya simu ukanitumia
Nikashukuru ndoto yangu ya pili ikawa imetimia
Hizi hisia zangu za kweli
Ndoto zangu mbili zimetimia
Nisaidie ya tatu isifeli
Naomba uelewe kuwa nakupenda kiukweli
Hizi ndio hisia zangu za kweli Msodoki

Nimeamini ndoto yangu ni we (we wee)
(Ni we unaenifaa)
So me Insta Message imefanya ni-fall inlove
Fall inlove (wee)
So me Insta Message imefanya ni-fall inlove
Fall inlove

Kabla sijafanya mengi kwenye uwanja wako
Naomba niwe mmjenzi
Hapa sahivi naongelea mapenzi
Sitosikiliza washenzi naamini mi ni chaguo
Ntaekufaa hata kama wanaokutaka wengi
Picha zangu usihofu mi ni hustler kidume
Warembo nilowa-post ni wanangu wala usifikirie kinyume
Tunda juu ya mti sina budi nikuchume
Na nimeona picha zako waga hu-post wanaume
Insta Message usiwaze ukaniona sina maana
Ukahisi nimetongoza wengi kwanza nime-download jana
Kwa ajili yako mama
Endapo ukikubali nitaifuta maana sijajua kuitumia sana
Upendo wangu ni we furaha yangu ni we
Ingawa nahofu ’cause nangoja jibu lako we
Naomba uelewe mi nakupenda kiukweli
Hizi ndo hisia zangu za kweli Msodoki

Nimeamini ndoto yangu ni we (we wee)
(Ni we unaenifaa)
So me Insta Message imefanya ni-fall inlove
Fall inlove (wee)
So me Insta Message imefanya ni-fall inlove
Fall inlove

Fall inlove

Hahaha
(Fall in love)
Hizi hisia zangu sidhani kama nakufuru
Kiukweli kabisa mi nakupenda
Na nategemea jibu zuri kutoka kwako
Your one and only
Young Killer Msodoki
I love you

Toa Maoni Hapa

SHIRIKISHA MWINGINE

Your email address will not be published. Required fields are marked *

SHIRIKI KUONGEZA MISTARI