MISTARI YA WIMBO HUU

Yoh!
Sio kila Young ni Killer, uwezo utajieleza
Na sio kila sharobaro imeandikwa atafia Muheza
Vaa, pendeza, nenda disco cheza
La mwisho utambue mkufu hausimami hata ulishwe pweza
Nipe kipaza Msodoki kama unaitaka shughuli
Nilikotoka hakuna noti vipi nisote na sifuri
Loki nyeti zako kwa kufuri acha kiburi
We demu unaelia huku unaikoki pisto ya Dully
Naeza kubuni au ku-copy na ku-paste
Mi muhuni ambae toka vidudu nalala gesti
Usijaribu au ku-test
Kwa Mwanza, ukinitoa mimi na Fid, Kadigo ndo rapper best
Ama Kambeshoga, maana unanishangaza
Kwako inanoga ila si Jakaya kakataza
Mombasa wanakuwaza, amini blaza kama pesa mawe
Jiji tajiri lingekuwa ni Mwanza
Wanashangaa eti wapi natoa rhymes
Huu ndo muda wa mastailasi ina maana Startimes eeh
Mi ni mshamba wa Mwanza Mwanza kwenye pori
Ila demu wako anipe namba atakusimulia magori

I do me kwani hata nilivyoanza walisema mi ni kitu gani
Siwasikii bado nasonga nakimbiza haijalishi natoka city gani
I’m so yeye yee (Young Killer, Mwanza Mwanza)
Wowo woh (Stamina, Moro Town)
I’m so yeye yee (Mbeya City, stand up)
Wo wo (wo woo)

Ah!
Mnaojiita wakali hizi salamu ziende kwenu
Mi ndo yule MC hatari ninaeogopwa na baunsa wenu
Siogopi shari, snitch diss nilete kwere
Mi nina mistari mikali hadi Rwanda ananionea gere
Tega kichwa ili upate mistari kwenzi
Na maujanja yasiojificha kama lafudhi ya kizenji
Mjenzi wa tenzi nae jenga jengo la rhymes
Vichwa panzi hawaniwezi kwa ukwezi wa hizi bumps
Dondosha chozi kama una jicho la huzuni
Hili ndo kovu la ngozi halifutiki kwa sabuni
Mziki nimeuanza kale hadi leo sijaitwa Pepe
Kipofu mwenye machale naijua hadi chuma-ulete
Pusha kaa mbali mentali sivuti kush
Nina mistari mikali hadi George anarudi bush
Beki umechoma timu yetu hatukupi ndondo
Daily narusha mangoma kama naundugu na Msondo
Ndoa ngumu na mke mwema sijapatiwa
Japo mke wa mtu sumu ila ghetto nina maziwa
Siuzi kwa mdosi ila loss inanipa lecture
Bongo jua la utosi hadi Juma anakosa nature

I do me kwani hata nilivyoanza walisema mi ni kitu gani
Siwasikii bado nasonga nakimbiza haijalishi natoka city gani
I’m so yeye yee (Young Killer, Mwanza Mwanza)
Wowo woh (Stamina, Moro Town)
I’m so yeye yee (Mbeya City, stand up)
Wo wo (wo woo)

Yoh!
Mi na moyo wa Young Killer, sina moyo wa subira
Shule sijawahi kufunzwa kwa chief ni Q Chillah
Ni zoom kwa taswira, verse zina hasira
Wengi wanaobebwa mwishoni ndo wanachezwa kama mpira

Wanaukubwa wa mwili ila akili saizi ya Diclopar
Uzito wangu wa mashairi haushushwi kwa chupa ya Vodka
Njiti wa vina niliyekua bila malezi
MCs wengi wa kichina bado wana ufeki wa tenzi

Ukiwa shujaa kama Young Killer, ku-win must
Watu wanalia njaa hadi Mwembe Chai hakuna breakfast
Nagawa tenzi na washenzi hawanipati
Wasionialika kwenye ujenzi eti kisa nakula bati

Sitemi kimombo hii ni bombo yenye krati
Mnenguaji rudi Congo hii ndombolo ya kimang’ati
Beat inavuja damu nimeibaka bila huruma
Mziki vita ya kalamu ni mwiko kurudi nyuma

Ukiniacha tunda mnafki utakula maganda
Ukifa umelala hauwezi ukazikwa juu ya kitanda

Sijilindi na ustaa, najikinga na ukimwi
Naogopeka kila mtaa kama nilizini na zimwi

I do me kwani hata nilivyoanza walisema mi ni kitu gani
Siwasikii bado nasonga nakimbiza haijalishi natoka city gani
I’m so yeye yee (Young Killer, Mwanza Mwanza)
Wowo woh (Stamina, Moro Town)
I’m so yeye yee (Mbeya City, stand up)
Wo wo (wo woo)

Toa Maoni Hapa

SHIRIKISHA MWINGINE

Your email address will not be published. Required fields are marked *

SHIRIKI KUONGEZA MISTARI