MISTARI YA WIMBO HUU

Thank you God it’s another day
I’m alive; no stress no pain
Yah let me work it out
Nahreel

We mwanadamu jaribu kujiuliza
Ungekuwa Mungu ni nani ungemsiikiza
Polisi wa doria au kibaka ndani ya giza
Je ni nani angepokea miujiza
Mlevi wa gongo au mama anayeuza
Yote tisa ungemponya mgonjwa ndani ya machela
Papii Kocha Seya wangegeuka Paulo Sila
Au ungelala na kuzuga hutuoni mafukara
Simba anakuomba wewe kabla ya kumuwinda swala
Swala anafanya sala umuepushe na misala
Je ungekumbuka kuwa mbu hajala
Ungemkumbuka Mwanaidd wa Mbagala
Tuma anakuomba wewe kabla ya kulala
Wakati jambazi sugu huko nje anafanya sala
Anaomba Tuma alale fofofo usiwe msala
Je ungenipa mke mwenye upendo kama Wastara
Au ungenisakizia changu mwenye penzi la biashara
Ungekuwa Mungu ungeshameza sumu
Au ungeshatuchoma moto kuyakwepaa majukumu

Jaribu kujiuliza jaribu kujiuliza
Je ungekuwa Mungu wooh uwooh
Je ungekuwa Mungu wee
Je ungelisha ndege wa angani wee
Je. ungetupa pumzi bure wee
Oooh wooh

Ungeijua kesho na kesho kutwa
Ungeshuhudia mkono wa albino ukikatwa
Na mkataji akikulilia asije kukamatwa
Ungekuwa Mungu nahisi ungeshadata
Kuna kina Mariam na Lamata
Wanataka ndoa na wachumba hawajapata
Mungu sina kazi na nataka kula bata
Je kweli ungemkumbuka yule ndege wa Tabata
Wajane yatima wasingechoka kukufuata
Wacheza kamari maimamu na mapasta
Mgonjwa anaomba apone mapema
Wakati muuza jeneza alikulilia mapema
Muuguzi anasema baba huyu mgonjwa usimponye mapema
Nina shida na kiasi cha hela kwa ajili ya mama
Nahisi ungehisi tunakusakama
Kina sisi tunaotaka riziki kwa kuchana
Mwanafunzi analia mimba itolewe
Wakati mgumba anakesha macho na mumewe
Vipi sasa Mungu ndo ungekuwa wewe
Kifaranga anatembea akikuomba wewe
Sikia maombi juu ya mwembe chakula anataka mwewe
Ungeyasikia maombi ya kichaa
Au ungekomba pesa zote halafu ukakesha bar

Jaribu kujiuliza jaribu kujiuliza
Je ungekuwa Mungu wooh uwooh
Je ungekuwa Mungu wee
Je ungelisha ndege wa angani wee
Je. ungetupa pumzi bure wee
Oooh wooh

Ungeficha siri zako kama nguo za ndani
Au tungeona kila kitu ka daktari wa labour
Je ungeyasikia maombi ya kahaba
Anayesali kabla ya tendo umuepushe na miwaya
Au mwasherati anayezuga mwanakwaya
Ungetupa shavu kama Mungu wa Isaya
Maana bila wewe hakuna Kala wala Jeremiah
Ungesema haya ungewakumbuka wasukumaa na wahaya
Vipi lugha zao zingepanda hawa wala kaya
Vipofu wangeona Au ungedili na vigogo
Vipi mademu wa mjini wenye nyodo na mikogo
Je ungeichoma Sodoma na Gomola
Au ndo kwanza ungenogewa na ishu za mduara
Mamba ana njaa anataka nyumbu
Nyumbu anakuomba umuongoze mto usio na mamba
Wakulima wanalia lete mvua juu ya shamba
Dobi ndo katoka kuanika nguo juu ya kamba
Bila Mungu we siyo kitu achaa ushamba

Jaribu kujiuliza jaribu kujiuliza
Je ungekuwa Mungu wooh uwooh
Je ungekuwa Mungu wee
Je ungelisha ndege wa angani wee
Je. ungetupa pumzi bure wee
Oooh wooh

Yeah think twice
Natokea Mwanza

Toa Maoni Hapa

SHIRIKISHA MWINGINE

Your email address will not be published. Required fields are marked *

SHIRIKI KUONGEZA MISTARI