MISTARI YA WIMBO HUU

Nipeleke kwa mganga
Na mimi nataka wanga
Maana mapenzi yamenikoroga kinoma
Anichanje chale mwili mzima
Nisimkumbuke hata jina
Yule hasidi
Gaidi wa moyo wangu
Anichanje chale mwili muzima
Nisimkumbuke hata jina
Yule asidi
Gaidi wa moyo wangu

Haya mapenzi basi
Nimeyavulia shati
Kupendwa ni ajira
Na mimi sina vyeti
Haya mapenzi basi
Nimeyavulia shati
Kupendwa ni ajira
Na mimi sina vyeti

Kule kukusifia
Mabaya kukufichia
Mbele ya mama
Oh baba
Oh lala
Mapenzi sio ubondia
Najikaza huku nateketea
Bora nijivue
Nisijisumbue
Mapenzi sio ubondia
Najikaza huku nateketea
Bora nijivue
Nisijisumbue

Sasa basi (sasa basi)
Inatosha
Nimekopesha mwili wangu
Bila kuogopa
Kumbe jike shupa (shupa)
Hata kwenye karata haupo
Unaruka kila sehemu umeshapita
Sasa basi

Ulijidai kunipima akili kwa mizani
Kuniendesha kama toy
Kukosa nuru kisa kizani
Ukanikinai aibu kunitia hadharani
Kuniona sifai
Masikini nimekosa nini

Haya mapenzi basi
Nimeyavulia shati
Kupendwa ni ajira
Na mimi sina vyeti
Haya mapenzi basi
Nimeyavulia shati
Kupendwa ni ajira
Na mimi sina vyeti

Kule kukusifia
Mabaya kukufichia
Mbele ya mama
Oh baba
Oh lala
Mapenzi sio ubondia
Najikaza huku nateketea
Bora nijivue
Nisijisumbue
Mapenzi sio ubondia
Najikaza huku nateketea
Bora nijivue
Nisijisumbue

Sasa basi (sasa basi)
Inatosha
Nimekopesha mwili wangu
Bila kuogopa
Kumbe jike shupa (shupa)
Hata kwenye karata haupo
Unaruka kila sehemu umeshapita
Sasa basi

Yeap
What goes around comes around baby
Mr T-Touch
Nuh Mziwanda
We pop anhaa
Mr T-Touch
Pop it
K Zone
You know how it is always and always
Anha hey yeap
Mziwanda

Inauma inauma
Inauma inauma
Inauma inauma
Inauma inauma

Toa Maoni Hapa

SHIRIKISHA MWINGINE

Your email address will not be published. Required fields are marked *

SHIRIKI KUONGEZA MISTARI

VIDEO YA WIMBO HUU