MISTARI YA WIMBO HUU

Ruka, jirushe
Acha kusita
Anha ruka
Ru-ruka, ruka
Anha

Kona zote za mji wote wametinga hapa
Wenye mavumba na wachumba ndo wanaochapa
(Hahah)
Nawe jirushe, jirushe
Wacha kusita ingia kati ujirushe
Mida inavyokwenda hali inazidi shamiri
Watu wanazidi ongezeka kama vile utitiri
Huwezi amini warembo walivyoumbika
Marashi yananukia utasema vile malaika
Oyoh Yoh njoo turuke wote
C’mon, ruka
Yoh njoo turuke wote
Ukiangalia vinywaji vimejaa counter zote
Mabibi na mabwana kwa mbwembwe wanaongozana
Masela nao wanapiga donee waweze kuzama
Parley ya leo imejaa
Imetawaliwa na furaha
Na hakuna mjinga yeyote ambae ataleta karaha
Endapo ntaikama stick ya pool table
Ntapanga hadi mwisho nkiiwakilisha Bongo Record label
Mkononi, shingoni natisha bling bling kachaa
Mkono mmoja glasi ya whisky
Nyingine nimemkumbatia mamaa
Nawe jirushe, jirushe rushe

Jirushe, jirushe, jirushe rushe
Jirushe, jirushe, jirushe rushe
Leo kwa pamoja tumekusanyika
Na muda wa ku-spend sasa umefika
Masela ruka (aii)
Kwa mizuka (ai ai)
Ingia kati (aii)
Serebuka aa (ai ai)
Masela ruka (aii)
Kwa mizuka (ai ai)
Ingia kati (aii)
Serebuka aa (ai ai)

Niweke pembeni ustaarabu uombe samahani
Twende ukaone mambo yanayotokea usiku duniani
Au unataka demu
Wapo wembamba, wapo wenye mgongo
Au unacheza pool (okay)
Twende nikakuonyeshee kiwango
(Jirushe)
Kama unataka kwenda kwenu nenda
Wenzako wanajituma ili mradi wapige hata denda
Lakini ukumbuke mpira, usije ukaleta drama
Hapa hakuna demu wa kwenda nae nyama kwa nyama
Kama ulimi ni mzito, omba mtu akupige tough
Na baunsa akilewa toilet unakula pafu
Midudu inawake akiona umefikisha bia tatu
Hali inavyobashiri leo lazma atabebwa mtu
(Jirushe) dada zangu wa kisasa
Ndani ya jeans wamevaa G-strings
Mabishoo wamevaa midosho
Wanazuga eti blings
Jirushe kama unachako mfukoni sio cha mshikaji
Wananiita Moe Technique
Ukipenda Mbakiaji, Jay Moe

Jirushe, jirushe, jirushe rushe
Jirushe, jirushe, jirushe rushe
Leo kwa pamoja tumekusanyika
Na muda wa ku-spend sasa umefika
Masela ruka (aii)
Kwa mizuka (ai ai)
Ingia kati (aii)
Serebuka aa (ai ai)
Masela ruka (aii)
Kwa mizuka (ai ai)
Ingia kati (aii)
Serebuka aa (ai ai)

Mademu kwenye dancefloor
Ebu nyoosha mikono yenu juu, mikono juu jirushe
Na machizi kwenye dancefloor
Ebu nyoosha mikono juu, mikono juu tujirushe eeh
Tujirushe ee eh
Ntarara ntararara, hey hey
Sasa umefika muda wa kuingia kati mmoja mmoja
Kwanza ngoja nacheza kwa P kisha mi naanza vioja
Mi na masela wangu
Wazushi na kama kawaida wanapiga virungu
DJ anavyou-mix, aliopia anauchengua umati
Hip Hop, Bolingo, Mduara na Ragga Mafin
Mpenzi, napokwenda nawe nifate
Nikikukumbatia nawe mabega nikamate
Usiwe na wasi usafiri wa kuondoka nje upo
Nipo na wewe leo sina habari na milupo

Jirushe, jirushe, jirushe rushe
Jirushe, jirushe, jirushe rushe
Leo kwa pamoja tumekusanyika
Na muda wa ku-spend sasa umefika
Masela ruka (aii)
Kwa mizuka (ai ai)
Ingia kati (aii)
Serebuka aa (ai ai)
Masela ruka (aii)
Kwa mizuka (ai ai)
Ingia kati (aii)
Serebuka aa (ai ai)
Jirushe, jirushe, jirushe rushe
Jirushe, jirushe, jirushe rushe
Leo kwa pamoja tumekusanyika
Na muda wa ku-spend sasa umefika
Masela ruka (aii)
Kwa mizuka (ai ai)
Ingia kati (aii)
Serebuka aa (ai ai)
Masela ruka (aii)
Kwa mizuka (ai ai)
Ingia kati (aii)
Serebuka aa (ai ai)

Eyo, si utani
Majani, Marijani
Bongo Records, kwenye fani
Au sio

Toa Maoni Hapa

SHIRIKISHA MWINGINE

Your email address will not be published. Required fields are marked *

SHIRIKI KUONGEZA MISTARI