MISTARI YA WIMBO HUU

Huu moyo huficha siri ambazo kwa macho huzioni
Kwa kuwa mi si mchoyo ntakupa jambo jipya sikioni
Fadha zao ni nyingi nyingi zaidi ya akili zao kichwani
Hawasikilizi shida zako za msingi nao wana zao
Mnazi haupandwi kwa ukucha
Na mpanda ngazi hushuka
Kuteleza sio kuanguka, mbaya ukishindwa kunyanyuka
Anaefanya hajui chochote, anaejua hawezi fanya
Ambae amechoka kufikiria huamini anajua sana
Kama hujutii ya jana na pia hauhofii ya kesho
Unaweza kuyapatia kimaisha, yeah, au kuyaotea
Unataka kuchukiwa na mjinga?
Mwambie akikosea
Ukweli siku zote unapigwa pingu uongo uzidi enea
Wenye nia hawana nguvu, na wenye nguvu hawana nia
Wanaridhika na moja, wanaogopa kutafuta mia
Wanayafokea maji wakati wanaogelea
Ukiwakosea hawa-press charges, vidole vyao vimeenea
Uzembe umewafelisha wengi na bado wengi wanatega
Wanaumia hii dunia imewaangukia juu ya mabega
Na wakilega wanakosa hata food juu ya meza
Sina budi (kuwaeleza)
Hizi ndo juhudi za wasiojiweza

Umewafelisha wengi na bado wengi wanatega
Wanaumia hii dunia imewaangukia juu ya mabega
Na wakilega wanakosa hata food juu ya meza
Sina budi (kuwaeleza)
Hizi ndo juhudi za wasiojiweza

Moyo nakwambia tizama ukihisi
Usicheze na nyunda usojua usi
Mzoea punda, hapandi farasi
Hapandi farasi kwake si mzuri
Japo mlabichi nguo za hariri
Huona najisi, si yake fahari
Si yake fahari kweli nakwambia
Nguru kwa ugali, amemzoea
Ziwa kwa sukari, ukimpa hulia
Ukimpa hulia kasikitika
Dole hujitia kayatapika

Juhudi za wasiojiweza

Wanajifanya wanaleta msaada kumbe wanaingiza madawa
Mtwara tutakula wapi ndo kundi la kwanza kupagawa
Wanatumia antidote kabla ya kukumbana na sumu
Kuanzia unyayo hadi utosi, nje ndani utajilaumu
Hata dunia iki-change vipi paka hawezi taga mayai
Na ukiyachemsha, ukiyakaanga haupati vifaranga, right?
Wanamrudisha ndani ya maji samaki aliyekufa afufuke
Kamba iliyolegea, kama una haraka usiivute
Dini zinageuzwa kuwa biashara kubwa kubwa huwezi amini
Wanajaribu kutuangusha wanakuta tushalala chini
Kuna masikini na omba omba wanaogeuza kidonda mtaji
Kuna ukimwi na siamini wagonjwa ndom waliitumiaje
Anaezijua lugha tofauti kote atapaona nyumbani
Fanya uzijue na kona zote ka ufagio wa zamani
Amani ilileta pesa, pesa imeleta vita
Hawazingatii mauzo ya wasanii baada ya kulipwa
Ni vyema kumpenda mkeo, siri zako umwambie mama ‘ako
Usijemuonyesha utupu mkweo kisa umelewa itakuwa aibu yako
Mlevi kesho yake hujuta zinapomruka hana hata jiti
Au labda alipigwa chupa, baa za siku hizi ugomvi wa viti
Emcee mkali hushuka mzuka wa mistari kwa ubovu wa beat
Au anapoirusha track kali DJ haipigi
Emcee mkali hushuka mzuka wa mistari kwa ubovu wa beat
Au anapoirusha track kali DJ haipigi

Juhudi za wasiojiweza
Juhudi za wasiojiweza

Toa Maoni Hapa

SHIRIKISHA MWINGINE

Your email address will not be published. Required fields are marked *

SHIRIKI KUONGEZA MISTARI