MISTARI YA WIMBO HUU

Mrembo, njoo tujenge malengo
Nikikutazama naona nyufa kwenye mjengo
Unaonekana kama mji wenye upendo
Unafanana na mtu alochoshwa na mwendo
Si nikupe namba yangu unipigie weekend?
(weekend, weekend baby)
Moyo unasema mchukue huyu mtoto yuko
stendi
Vile anavyohema sio kama mtu hapendi
Anauelewa mziki anahofia kuucheza
Anasema na lugha chafu, ameshakuwa Kifimbo
Cheza!
Sema nini na Marlaw nabembeleza
Kwa sera za Suma Lee nakula chungwa mpaka
chenza
Ehee, shida kujiuguza
Mama yu hot na uko ndani unaniunguza
Staki kujua, hata nikijua ntapuuza
Ukitaka kula bata uache kumchunguza
Aah! Kama utanipenda
Sitojali shida ulizobeba
Na kama unataka kucheza
Katafute refa wa kukubeba
Na kama utanipenda
Sitojali shida ulizobeba
Na kama unataka kucheza
Katafute refa wa kukubeba

You know I like you
Mi nakupenda and I give you what you want eh
(eeh whatchu want)
Nipe uchizi nidate
Hata nikilale kwenye usingizi nifate
(The way you talk mama)
You know I like you
Mi nakupenda and I give you what you want eh,
baby (eeh whatchu want)
Nipe uchizi nidate
Hata nikilale kwenye usingizi nifate

Ha kuna single wala movie, mama you’re my star
Mi shabiki yako nasimama hata ukikaa
Nahangaisha paa, breki ziko Dar
Jitazame kwenye kioo how beautiful you are
Mapenzi ukichaa, mapenzi uchizi
Uwe nacho ukikataa, mwingine inamnyima
usingizi
Mwingine atakesha, mwingine atatesa
Mwingine atataka akutumie kama pesa
Yanajuana madini yakikutana
Mwanamke ntanyima tuzo na ndo kitu
nachofanya
We utasema mi kichaa
Kumbe mwenzako nafata what I feel inside
Aah! Kama utanipenda
Sitojali shida ulizobeba
Na kama unataka kucheza
Katafute refa wa kukubeba
Na kama utanipenda
Sitojali shida ulizobeba
Na kama unataka kucheza
Katafute refa wa kukubeba

You know I like you
Mi nakupenda and I give you what you want eh
(eeh whatchu want)
Nipe uchizi nidate
Hata nikilale kwenye usingizi nifate
(The way you talk mama)
You know I like you
Mi nakupenda and I give you what you want eh
baby (eeh whatchu want)
Nipe uchizi nidate
Hata nikilale kwenye usingizi nifate

(Unataka nini mama?)
Usiniumizi moyo (waweza kupaa)
Mi niko loyal (uendeshe motor car)
Punguza uchoyo (nguo za kuvaa)
You’re my everything for me (Na ukiwa out,
order what you want)
(Waweza kupaa) baby
(Uendeshe motor car)
(Nguo za kuvaa)
(Na ukiwa out, order what you want)

You’re my everything for me
You’re my only one

Toa Maoni Hapa

SHIRIKISHA MWINGINE

Your email address will not be published. Required fields are marked *

SHIRIKI KUONGEZA MISTARI