MISTARI YA WIMBO HUU

Ntampata wapi kama yule
Mwenye tabasamu kama lile
Nimpende anipende
Awe wangu maishani
Shida zake ziwe zangu
Shida zangu ziwe zake
Tabu zake ziwe zangu eh
Tabu zangu ziwe zake

Nampenda mwenye afya
Namuogopa wa maradhi
Anipende kama mimi
Anipende kwa makini
Nimpende kwa makini
Nimpende kama mimi
Awe simple kama mimi
Hakika nithamini
Moyoni ntampokea kwa hali yoyote
Na yeye anipokee basi kwa hali yoyote

Ntampata wapi kama yule
Mwenye tabasamu kama lile
Nimpende anipende
Awe wangu maishani
Shida zake ziwe zangu
Shida zangu ziwe zake
Tabu zake ziwe zangu eh
Tabu zangu ziwe zake

Aniliwaze kama yule
Kwa utamu wa mapenzi
Aniliwaze kama yule
Kwa utamu wa mapenzi
Aniliwaze kwa sauti kama ndege angani
Na marashi ya Zanzibar ajifukize na udi
Chumba chote kinukie
Mpenzi wangu nimpende
Anibusu nimbusu nikumbatie mpenzi
Nami nikukumbatie tuoneshane mapenzi
Tucheze cheze kitandani ishara ya mapenzi
Tucheze cheze kitandani eh ishara ya mapenzi
Anapolia nimbembeleze
Akilia nimbembeleze
Napolia anibembeleze
Hapo mimi ntatulia
Kama ndege kwenye juni
Hapo mi nitatulia ah

Ntampata wapi kama yule
Mwenye tabasamu kama lile
Nimpende anipende
Awe wangu maishani
Shida zake ziwe zangu
Shida zangu ziwe zake
Tabu zake ziwe zangu eh
Tabu zangu ziwe zake

Ntampata wapi kama yule
Mwenye tabasamu kama lile
Ntampata wapi kama yule
Mwenye tabasamu kama lile
Ntampata
Ntampata
Ntampata wapi kama yule
Twende twende
Twende sasa tuimbe wote
Ntampata
Ntampata
Ntampata wapi kama yule

Ntampata wapi kama yule
Mwenye tabasamu kama lile
Nimpende anipende
Awe wangu maishani
Shida zake ziwe zangu
Shida zangu ziwe zake
Tabu zake ziwe zangu eh
Tabu zangu ziwe zake

Toa Maoni Hapa

SHIRIKISHA MWINGINE

Your email address will not be published. Required fields are marked *

SHIRIKI KUONGEZA MISTARI