MISTARI YA WIMBO HUU

Karata Dume – Afande Sele na Mez B

Yo yo yooh
Unaona eh
Karata dume
Na Simba Dume
Toka Bongo Record
Na Mez B wa Area C

Babaake Tunda jema naicheza karata dume
Ndo manake kiutu uzima naonyesha maana ya ufalme
Hakuna kuumiza kichwa
Eti nimpange nani wakati mimi ndo kocha
Ukipenda niite Galacha, Ticha
Ama kwa heshima ya rasta unaweza kuniita Culture
Kama nnavyowakilisha kwa masela wa chaukucha
Tangu nashtuka kwa pusha mpaka siku nilipoacha
Si unaelewa kitambo watu wanastua
Sema dozi inapungua jinsi umri unavyokua
Ujana una mambo mengi
Ndo sababu mara nyingi unakosana hata na dingi
Lakini ukishakuwa mkubwa
Bahati mbaya we ndo mama we ndo baba
Ukicheki usawa unakaba
Unaona yes kachala ngoja ntulie
Maana nikienda resi kifala ntakufa mie
Mambo hayajawa dangachee
Bado msanii wa bongo sitendewi haki daily
Muziki wangu naibiwa
Mwizi wangu namjua
Sema ntafanya nini mheshimiwa hajaamua
Kuonyesha yuko pamoja na mimi tumvunje chawa
Msanii nadhulumiwa
Kazi nafanya mimi bei ya kuuza napangiwa
Nikibisha narudishiwa
Utauza wapi
Useme ukomae mwenyewe kibongobongo hailipi
Mara ngapi wangapi waliuza wenyewe mwishoni wakakwaa visiki
Uliona wapi msaii afanikiwe pasipo haki miliki
Labda utajiri wa kibongo
Kuwa vyumba viwili uswahilini na gari ndogo
Kwa mimi hainipi jeuri kuona tayari
Nianze kuimba manyimbo ya party rastafari

Naicheza karata dume
Mapema kuimarisha ngome (hold on)
Naicheza karata dume
Nasema jahazi lisizame (fire)
Naicheza karata dume
Mapema kuimarisha ngome (fire)
Naicheza karata dume
Nasema jahazi lisizame (hold on)

Toa Maoni Hapa

SHIRIKISHA MWINGINE

Comments are off this post

SHIRIKI KUONGEZA MISTARI