MISTARI YA WIMBO HUU

Niliamini mapene hayatoshi
Na niki-hustle siyakosi
Sababu sipo kwenye loss na life simple huwa hai-cost
Kwahivyo nikaenda Dar na train of thoughts
Sikwenda kuzubaa au kushangaa ni kusaka chapaa boss
Sikutaka kuivaa mikosi nilitaka kuivaa mikoti
Sikuwa na passport password pin lakini nili-crack codes
Walioni-support wote siwaoni kwa line
Wakini-approach ili nifungue pochi ya noti tu-shine
Hatuko fine

Je mimi ni kaka mubaya
Kaka haso haya
‘Kaka’ huniitaga Nakaaya
Mama C huniita brother bila shaka Mozaya
Niko sick and tired of being sick and tired

Na huu ni mwaka wa ndui
Sitaki upele urudi tena mnachotaka sikijui
Nashukuru hamtopata mbawa ikiwa mtaupata huo uchui
Mnautaka uadui
Mnayempaka ni mtata makaka hamkui
Mmeendekeza hila legeza hasira za harakati
Mie nita-ball hata kwa mpira wa makaratasi

Unaweza ukahisi mie napita tu kwa kusahau mie nina-hustle
Nimezaliwa Afrika ugumu wa maisha umenifunza ku-struggle
Ukiwa idle unamu-attract shaytwan
Kichwani nina Msahafu na Bible life ni zaidi ya ku-have fun
Kwani kila kicheche anajiona ni mzima
Na njia pekee ya kuepuka ngoma ni kugoma kupima
Ikiwa maujuzi haya hayakugusi itanilazimu nikuelewe
Sometimes hata kamusi hui-miss tafsiri yenyewe

Nalindwa na dua za mama tangu baba simjui
Namfanya adui mwenye njama aache drama na akue
Ili ajijue kabla hajakwama huko mrama asitue
Ajikwamue kwenye lawama yenye maana yamchukue
Kisha aniombee mimi ili nifaidike kwa hizi mbio
Siamini kwenye umasikini hivyo sihofii mafanikio
Ndiyo mie ni leo kwahiyo sifikirii kushindwa
Zingatia kauli hiyo hausikii inaashiria ubingwa
Mie ni mbishi muulize Nikki hatopinga
Na hata kama ningekua mbuzi ningelala chaka la simba

Toa Maoni Hapa

SHIRIKISHA MWINGINE

Your email address will not be published. Required fields are marked *

SHIRIKI KUONGEZA MISTARI

VIDEO YA WIMBO HUU