MISTARI YA WIMBO HUU

Kwa sifa moja umenikamata
Nakupa we peke yako ndo umeniweza
Nilikopita nimeteleza
Lakini kwako we ndo kiboko yangu

Kila shetani ana mbuyu wake we ni mibuyu mitatu
Ukiamua unitumikishe mwenzio ntalala na viatu
Najionea maajabu najionea mapya mama angu
Hakuna mapenzi ya hivi popote kwenye ulimwengu
Siwezi elezea jinsi navyokuzimia
Nikicheza na moyo wako unacheza na wangu pia
Nafsi yangu ilishapotea siwezi hata kujitetea
Ka ulitoroka peponi uzuri ulivyokuenea
Piga la kushoto ntageuza na la kulia
Wengine hawanijaribu wanajua kitakachotokea
Sitaki mambo yaende kombo na yakienda yawahi kurudi
Hatuendi nayo hatuwezi shindwa yaje na mapambio ikibidi
Tunapishana hatugombani then we back here
Hatuendi juu hatuendi chini love we right here (oh)
Hata mapenzi yakifa boo si tubaki sawa tu
Si ni watu wazima love hatuwezi kuishi ka underground
Ujue una nusu ya moyo wangu na nusu ilo baki kwangu
Yote nakupenda wewe una jua langu una mwezi wangu
Unatembea na roho yangu (wewe)
Sio mtu tena wa mademu we ndo Michelle Obama wangu

Kwa sifa moja umenikamata
We peke yako ndo umeniweza
Nilikopita nimeteleza
Lakini kwako we ndo kiboko yangu
Sipagawi hawajui kwanza
We namba moja umewakimbiza
Unatembea na roho yangu
Nataka ujue we ndo kiboko yangu

Wakikuita vikao vya hino wambie uko busy na bwana
Na ubize hauwezi kuisha maana una mengi ya kufanya
Hatuwezi kosa usingizi sababu watu wanasema
Wana midomo waifanyie nini
Waache wakichoka wataizima
Uko mikono salama ’cause nakuzimia sana
Ka mboni yangu ya jicho jinsi navyokutazama
Mahaba to the moon and back
Kau keep it real kwa kifupi mambo ya kihuni sitaki
Nataka tuzeeke pamoja
Mpaka vikongwe mi na we bega kwa bega
Chochote unachotaka nime mipango ya kukupa kweli
Kama sina ntatafuta na naamini utasubiri
Huwezi omba ndege una akili huwezi omba meli
We ndo mtunza hela zangu utaomba unachoweza himili
Ka mteka meli wa kisomali we ndo captain wangu
We ndo suka man we ndo pilot love
Ujue una nusu ya moyo wangu na nusu ilo baki kwangu
Yote nakupenda wewe una jua langu una mwezi wangu
Unatembea na roho yangu (wewe)
Sio mtu tena wa mademu we ndo Michelle Obama wangu

Kwa sifa moja umenikamata
We peke yako ndo umeniweza
Nilikopita nimeteleza
Lakini kwako we ndo kiboko yangu
Sipagawi hawajui kwamba
We namba moja umewakimbiza
Unatembea na roho yangu
Nataka ujue we ndo kiboko yangu

Toa Maoni Hapa

SHIRIKISHA MWINGINE

Your email address will not be published. Required fields are marked *

SHIRIKI KUONGEZA MISTARI

VIDEO YA WIMBO HUU