MISTARI YA WIMBO HUU

Mazuu On The Beat
Uh uuh
Uh uuh
Mmh

Yale maneno matamu nikafikiri nyota njema
Mara asubuhi asubuhi moyoni
Kumbe miale ya sumu ulikusudia kunichoma
Angali sijui sijui kisa niii

Nimeamini penzi penzi zigo la miba
Lishanichoma na kunipofua moyo (moyo moyo)
Bila ye siwezi mwenzenu napata shida
Amani sina kinauma kidonda changu

Kitachelewa (uuh uh)
Kupona kitachelewa chelewaa
Sema kitachelewa sweetie
Kidonda changu
Kitachelewa (uuh uh)
Kupona kitachelewa chelewaa
Sema kitachelewa sweetie
Yarabi moyo wangu

Yale mahaba ninyonge ntayamiss saana si unajua
Umenifanya nikonde shilingi sina ningenunua
Umenipora hata tonge angali shibe sina utaniua
Ningekunywaga na pombe ila kichwa sina ningezimia

Nimeamini penzi penzi zigo la miba
Lishanichoma na kunipofua moyo (moyo moyo)
Bila ye siwezi mwenzenu napata shida
Amani sina ninaugulia kidonda changu

Kitachelewa (uuh uh)
Kupona kitachelewa chelewaa
Sema kitachelewa sweetie
Jamani kidonda changu
Kitachelewa (uuh uh)
Kupona kitachelewa chelewaa
Sema kitachelewa sweetie
Yarabi moyo wangu

Mmh
Na tena sipati usingizi (ai moyo ai moyoo)
Ati kula mi siwezi (ai moyo ai moyoo)
Tena nusu niwe chizi (ai moyo ai moyoo)
Yote kisa mapenzi (ai moyo ai moyoo)

Mazuuuuu (Record)
Maximizer
Harmonize baby

Toa Maoni Hapa

SHIRIKISHA MWINGINE

Your email address will not be published. Required fields are marked *

SHIRIKI KUONGEZA MISTARI

VIDEO YA WIMBO HUU