MISTARI YA WIMBO HUU

Mistari ya Kijiwe Nongwa – Rostam na Ney wa Mitego

Is another one
Take five now (take five now)
Bin Laden

Alikuja kama masihi tukamchangia sadaka
Tukamwona nabii aliyeshushwa siku ya Pasaka
Tukamtolea na zaka ili kanisa lijengwe
Eeh eh na bado akamlaza muumini kifo cha mende
Hivi unamkumbuka babu
Babu wa Loliondo
Ah-ah yule mfugaji mwenye bleach la Kikongo
Watu wamekufa watu wamefungwa watu wamepoteza biashara
Sasa umekaribia uchaguzi amerudi chama tawala
Vipi dada yetu wa Igunga mmh simwoni udangani
Ah mbona ashapata mchumba sio viben 10 wa zamani
Yule fundi gereji chawa si kamteka bibiye
Na wamefungua mgahawa yaani wote mama ntilie
Na kuna dem aliyeachiwa mtoto
Akaolewa na mtoto
Akaachana na mtoto
Akabaki anamlea mtoto
Hizi ndoa za mjini bwana zinasikitisha
Eeh maana hufungiwa chumbani na huvunjikia Insta
So soka la Bongo linakwama wapi
TFF maanake nini
Tanzania Football Failure ndo nachojua mimi
Unamfukuzaje Amunike ili udhaifu wenu muuvuge
Wakati mlimpeleka mlevi ye akacheze namba ya Mkude

Nasema leo hakilali kiporo
Imeshakuwa kero
Ukuta tunavunja kwa tindo
Wameshapigwa guu wako telo Na kiki za kikolo
Majita tushapiga kishindo
Hili ni fagio la chuma
Linang’oa visiki
Safisha vichaka kwa moto
Simba kageuka duma
Jangwa halipitiki
Ukitufuata umetoa boko

Marehemu walimsema mnyonyaji kwani mziki una maziwa
Sasa Mungu kamhitaji na bado hajafanikiwa
Hivi unadhani ndani ya mjengo nani ataliziba pengo
Acha maisha yaendelee jasiri ameumaliza mwendo
Aliyeokota almasi mchangani alikuwa Miss Tanzania
Na aliyekuja inunua dukani ni Mganda aliyekuwa na nia
Ya dhati ila hapa kati wakatokea maharamia akawatumia
Ila mwamba ni mnyanyasaji wa kijinsia
Sa skiza man (hii) vipi shem mama Ivan
Ah tupo tupo tu ila hatupo ka zamani
Nawe vipi kwani mbona wife simuoni nyumbani
Hey chill man sina majibu deal done
Bungeni daily majanga viongozi wameishiwa mada
Hivi mbunge wako wa Tanga hoja zake unaziskiaga
Sa nitazisikiaje na ana spika mbovu za wanakijiji
Ila fundi wao anakuja soon kutoka Ubelgiji
Nabii Tito na Dr Shika tayari wamesahauliwa
Mwenzao Mariamu biriani anapika anapakuliwa
Bongo bwana ndo nchi inayosapoti sana ujinga
Utashangaa Amber Rutty kala shavu ubalozi wa kinga

Yaliyosemwa yamesemwa
Kazi kwenye mmezoea kutema
Wakitaka tuyajenge tena
Waambie muda sio rafiki mwema (yeiye iyee aah aah iyee)
Kusema kweli hatuchoki
Na kwenda jela hatuogopi
Tutabanana ata kama hapatoshi
Hatupindishi ata kwa dumba

Nasema leo hakilali kiporo
Imeshakuwa kero
Ukuta tunavunja kwa tindo
Wameshapigwa guu wako telo
Na kiki za kikolo
Majita tushapiga kishindo
Hili ni fagio la chuma
Linang’oa visiki
Safisha vichaka kwa moto
Simba kageuka duma
Jangwa halipitiki
Ukitufuata umetoa boko

Bin Laden

Toa Maoni Hapa

SHIRIKISHA MWINGINE

Your email address will not be published. Required fields are marked *

SHIRIKI KUONGEZA MISTARI

VIDEO YA WIMBO HUU