MISTARI YA WIMBO HUU

Nikiwa masikani nimesizi, nimekata ringi
Kama utani akapita binti
Nkasita kumuita, kisa nyuma kafungasha
Nikawaza ntafika vipi
Mara akili fasta ikanituma
Songa nyanyuka, nikaanza kumfata kwa nyuma
Huku nikiwaza niseme nini
Ambacho atakubali ili mradi asiniteme mimi
Mwendo kwa mwendo mpaka stendi alipofika
Mrembo analipa lazima change utarudisha
Yuko simple na ana-hang kama sneakers
Mi niko hoi chini ni-bang na ma slippers
Ikiwa bado kasimama, anatizama
Basi lenye siti lije aweze kuzama
Sikupoteza mida, nikatinga
Nikamuuliza dada habari akajibu salama
Si unajua tena naishi kwa street
Sound nyingi mtoto dakika mbili aka-tick
Tukaachiana namba, gari likaja akapanda
Na hapo ndipo alipouanza mziki
Mara anaomba vocha, ukituma ana-beep
Ukipiga anasema haijatosha
Hii sasa inanichosha
Maana nishatumia zaidi ya milioni na bado sijatoa posa
Songa

Darling, leo ni birthday ya rafiki yangu
Na sijaenda hata shopping
I need money!

Yeah, daily mizinga mingi
Hii sasa imezidi, hata kama mwana sina dhiki
Yaani shopping kila wiki?!
Hadi nakosa raha ka rapper mbovu anae-flow bila beat
Nabaki mdogo ka Kirikuu
Kingine cha siri ni kwamba hataki ni-do
Ee hii sasa ni kuu, anata gari hajui usafiri wangu miguu!
Mara oh Songa nataka unijengee ghorofa
Kama huwezi tafuta hata bodi ya kuikopa
Si unajua uswahili mwenzako mi naogopa
Juzi wamevunja mlango wamesepa na zile sofa
Usitoshe kuna wachawi, usiku mi nawaota
Yaani ikishindikana tafuta mjengo mwingine Posta
Dah, mchizi nabaki nachoka
Nikikataa anasema najibu kilord Loffa
Kiukweli napata sana uchungu
Najiuliza hivi hana wazazi? Hata ndugu?!
Mara kila tukikutana virungu
Vingine siwezi kumpa inabidi kumuomba Mungu
Hivyo ni baadhi ya vitu anavyotaka
Ila viko vingi nikisema sitomaliza sasa
Kwa hali hiyo mwenzenu nime-surrender
Kama mapenzi ndio hayo basi mi sijui kupenda

Toa Maoni Hapa

SHIRIKISHA MWINGINE

Your email address will not be published. Required fields are marked *

SHIRIKI KUONGEZA MISTARI