MISTARI YA WIMBO HUU

Waswahili washasema shughuli kumchezesha Young Killer ngoma ya watoto
Ona wanavyohangaika kama wamemeza ugali wa moto
Bongo Nyoso
Walisema wakubwa
Mswahili hata akose company vipi sehemu yoyote hawezi kwenda na muda

Akili haifanyi kazi bila kuwa na maarifa
Mwanaume kwenye kazi huwaga silewi sifa
I’m the best sijasubiri nikifa
Nazichana top 10 niite Doggy wa Latifah
Popote kambi ukiniweka natusua
Na ukweli sio dhambi dhambi ya uwongo kuyazua
Aah unafuga kitambi hilo si jipu ungetumbua
Mama angu na chambi chambi za kuuza vitumbua
Anatulea tunakua unajifanya unatujua
Aah unatujua
Aah unazingua
Mic kama mtaji bila hii sifanyi
Mungu kanipa kipaji kweli sidanganyi
Mapenzi na kazi mmh kweli sichanganyi
Na mi na dogo dogo kweli hatufanani
Harufu kama choo nasaka dough kila mahali
Flow inakaba koo ni soo bila kabari
Bizzy Babylon niite upepo unapovuma
Nachana kwa microphone na mtoto wa kisukuma
Killer

Wacha si tufanye mambo kama yalivyo
Wacha si tupige dili kama zilivyo

Ni Msodoki na Baisa sa shituka
Waliolala wambie kumeshakucha

Wacha si tufanye mambo kama yalivyo
Wacha si tupige dili kama zilivyo

Ni Msodoki na Baisa sa shituka
Waliolala wambie kimeshanuka

Moyo hauridhiki sio mboyoyo za wanafiki
Nashangaa emcee mchoyo anavyogawa mashabiki
Ukiwa loyal unani-fit
Maana kwenye moyo ukizama umezama huogeli hata boya ulivae vipi
Ni Msodoki na Baisa
Aah stuka
Leo namtusi mamba kwenye mto na navuka
Sina wivu wala pupa
Maana ridhiki anaegawa Mungu ndiye anayetunyima na anaetupa
Naposikia beat kali ni raha tu
Hapo hisia zangu zina-enjoy iwepo ndani sayari ya tatu
Nakaza kamba za viatu wote wanatambua
Baada ya giza ni Young Killer anaongoza kuficha watu
Halafu hamuwezi niona mimi tu
Zingine mechi ngumu na dakika ni tisini tu
Siwezi uchukia umasikini
Duh
Japo siupendi
Ila shida ingekuwa sumu basi tungekufa wengi
Siku zinakwenda kama mbio za defender
Ila naomba Mungu nidumu kama nguo nisioipenda
Na demu mmoja nampenda
Sina skendo ya kugonganisha magari sijawahi kuwa daraja la Surrender
Kila kukikucha nakua uwezo unaongezeka najua
Mateso yakizidi ndo kutusua
Young Killer usicheze ngoma ya watoto
Ona wanavyohangaika kama wamemeza ugali wa moto
Nyoko

Wacha si tufanye mambo kama yalivyo
Wacha si tupige dili kama zilivyo

Ni Msodoki na Baisa sa shituka
Waliolala wambie kumeshakucha

Wacha si tufanye mambo kama yalivyo
Wacha si tupige dili kama zilivyo

Ni Msodoki na Baisa sa shituka
Waliolala wambie kimeshanuka

Toa Maoni Hapa

SHIRIKISHA MWINGINE

Your email address will not be published. Required fields are marked *

SHIRIKI KUONGEZA MISTARI

VIDEO YA WIMBO HUU