MISTARI YA WIMBO HUU

Tamaduni Muzik
Yeah
Combination Sound
Kombinenga

Siku ikifika tukubali
Tuwe macho
Kupanda na kushuka zote hali
Tuwe macho
Siku ikifika tukubali
Tuwe macho
Kupanda na kushuka zote hali
Tuwe macho

Vaa wema vua shari safari hatua
Round hii mbishi niko gengeni na jua kali
Siuzi nyanya vitunguu wala pilipili hoho
Too little too late ushachelewa Jojo
Wakiniona mi nashine wanachonga
Ndo maana kila line wanaponda
Vipi nikisign na Anaconda
Busy kwenye show mi nashow biz
Na kwa flow hizi si ndo time ya kusonga
Hahahahaaa
Hii ni hit ya kubaki
Mwenyei kaniumba fit ndo maana lift sitaki
Nabang kila session mpaka morning groove
Eti niko chini hunioni juu
Mi ni leader wa performing crew
Nizungue ubaki mweupe design ya hair style ya Monikuu
Haah Nikki Mbishi Songa One The Incredible
Komando Yosso ni mzozo ngoma ni terrible
Karibuni

Siku ikifika tukubali
Tuwe macho
Kupanda na kushuka zote hali
Tuwe macho
Siku ikifika tukubali
Tuwe macho
Kupanda na kushuka zote hali
Tuwe macho

Wanasema wanapenda vile mi hubonga kila kitu
Rap sonara madini huwa nachonga kila siku
Sina fleva za kibongo naonja kila kitu
Bila woga wanaloga niwe kioja kila siku
Kama unaipenda push play ama itose
Everyday iwe kush nei ama okay
Wazushi msichoke naghushi ninyooshe
Nipe changamoto sio kila nikigusa tu okay
Kuna watu wangependa nigote kwenye misele
Iwe kwere kote Moko nisote nisiende mbele
Nichoke niwe kero kokote au niende selo nisitoke
Ila msiogope nipo milele
Kwani muumba ndo mpaji kutunga kipaji
Niko macho wanataka kuniua niwe mtaji
Niko Anaconda na hii ndo ile siku niko mcaho
Ila wengi watakesha kila siku

Siku ikifika tukubali
Tuwe macho
Kupanda na kushuka zote hali
Tuwe macho
Siku ikifika tukubali
Tuwe macho
Kupanda na kushuka zote hali
Tuwe macho

Chungu kichungu natema sumu kisumu
Hali ni mgumu je utabeba dumu kidumu
Na kidumu mpaka wasaa utapotambaa
Na kushangaa kwamba kufika humu ni ngumu
Ukicheck chance hola
Unawaza utaishi vipi endapo majambazi wakipora
Basi bora
Kuwa na wasi kama polisi ni sawa na wazazi wenye bastola
Heeey
Na bado utakosa njozi
Kazi hakuna utanuna utashona gozi
Niite Songa endapo utakosa pozi
Au nyong’onyea zaidi ya mgonjwa aliyekosa dozi
We si kiongozi (ndio)
Mbona maji hakuna wananchi mtaani wanaoga chozi

Siku ikifika tukubali
Tuwe macho
Kupanda na kushuka zote hali
Tuwe macho
Siku ikifika tukubali
Tuwe macho
Kupanda na kushuka zote hali
Tuwe macho

Toa Maoni Hapa

SHIRIKISHA MWINGINE

Your email address will not be published. Required fields are marked *

SHIRIKI KUONGEZA MISTARI