MISTARI YA WIMBO HUU

Uh yeah
Mmh mmh
Yeah yeah
Uh uh

Kwanini umoja usidumu
Kwanini hizi nafsi bila uoga zihukumu
Kwanini hizi hoja zina sumu
Kwanini hii mizoga bila uoga ina tunu
Nauliza maswali majibu mbali yakiwa
karibu labda yatakuwa majibu shari
Kwenye hii hali ya mabwana na watwana
Hii ni Afrika haina Malawi haina Botswana
Mwokozi akiwa Yesu ukombozi unakuwa wetu
Wadokozi wachukua tusichojua ndo dua zetu
Tunafarakana huku karakana hazina fundi
Wanadamu wana vinywa vichungu ongeza chumvi
Wanaongeza sukari Muumba aongeza pumzi
Kwanini hawashukuru hii nuru bila kuruzi
Wahunzi hawaungi upendo wa kundi
Walevi waongeza tungi, niko naongeza utunzi

Why does it have to be that way
Why everything should turn that way
Why some people are still afraid
There should be a better way, to create a better day

Kwanini nawaza
Kwanini haya macho hayafumbi yaangaza
Kwanini hii sauti naikaza
Hapana Kwanini sauti naipaza
Kwanini dini Mungu mmoja sa tunatengana
Kwanini pesa ina mamlaka yenye uhasama
Tazama vijijini mmoja ana raha ishirini
Dhiki mpaka magonjwa yajaa usizini
Amani imekwisha kisa dini
Watu bila utu ila ukiamini hujiamini
Hakuna wa kumchunga zaidi ya ulimi
Hakuna wa kumvunja zaidi ya umimi
Ila pia nyinyi sio wakosaji vipi kwanini mnahukumu na mpo humu duniani wafitini
Maneno silaha, moto ka volkeno mitaa
Misemo inakaa ila ona kwenye meno kuna njaa

Why does it have to be that way
Why everything should turn that way
Why some people are still afraid
There should be a better way, to create a better day

Kwanini kila siku maafa ndo kila kitu
Kwanini kila kitu chakatwa kwa kila kisu
Kwanini hawa nyoka wazagaa kila msitu
Kwanini watakatifu watakashifu
Wata zidi dhambi kuna kambi za maovu
Hata hizi bangi sio chimbuko la makovu
Hizi rangi wanapaka, dhambi wanapata
Wapendezesha taswira kwenye jamvi la mashaka
Kwanini aagh
Kwanini wanadamu wana roho za kinyama
Wanyama ndo wana roho za kiungwana hizi zama
Vijana dhidi ya ujana
Usalama hauko salama, salama imebaki alama
Tazama shirika la umma lang’ata kabisa
Shirika la nyuma, shirika la buma mama huruma
Ka mshiriki wa hili shirika, shirika huna
Wema wanahema, wanasema bora tena
Kutokuwa mwema ni bora kuliko kuwa bora mwema
Ubora watetema, dola inapenya
Bora uwe tena kiumbe kipya, dunia mpya
Yenye wingi wa rehema

Why, why, why does it have to be that way
Why everything should turn that way
Why some people are still afraid
There should be a better way, to create a better day

Why yeh why, why
Some people are still afraid
To say what they feel in their hearts
There should be a better way, to create a better day

Toa Maoni Hapa

SHIRIKISHA MWINGINE

Your email address will not be published. Required fields are marked *

SHIRIKI KUONGEZA MISTARI