MISTARI YA WIMBO HUU

Lala salama
Matatizo, chuki, lawama

Ukilala lala salama, kumbatia picha yangu
Na kama ukinikumbuka sana nipigie simu yangu
Uki-ukilala lala salama, kumbatia picha yangu
Matatizo, chuki, lawama vumilia mpenzi wangu

Najua wivu ndo mapenzi, ila chunga usizidi
Si unajua kwako sijiwezi, ila dhiki mmebidi
Mi nilitamani sana mi kuwa nawe, tuwe wote usiku na mchana
Kilichonifanya mi nipagawe sina chochote cha kuwalisha wana
Niliupokea kwa unyonge msiba wa kaka Bonda
Ile barua yako ya mwisho ilinitonesha vidonda
Usije nilali kipenzi changu
Ukadhani nimekumbwa na pepo la starehe
Mambo bado magumu kwangu
Afadhali hata ya jana, ya kesho niombee

Ukilala lala salama, kumbatia picha yangu
Na kama ukinikumbuka sana nipigie simu yangu
Uki-ukilala lala salama, kumbatia picha yangu
Matatizo, chuki, lawama vumilia mpenzi wangu

Ile “kua uone”, nilidhani maghorofa
Ah aa kumbe mwana ukome, hakuna cha kuokota
Mi bado nakaza moyo changu kipenzi
Ila naumia kwa kuwa mwenyewe
Natamani ila siwezi, nazitafuta nije kula na wewe
Msalimu mama nyumbani, usisema kama nahenya
Tai, mfiche mpe imani, karibu ntakuoa chema
Usije nilali mpenzi wangu
Ukadhani nimekumbwa na pepo la starehe
Mambo bado magumu kwangu
Afadhali hata ya jana, ya kesho niombee

Ukilala lala salama, kumbatia picha yangu
Na kama ukinikumbuka sana nipigie simu yangu
Uki-ukilala lala salama, kumbatia picha yangu
Matatizo, chuki, lawama vumilia mpenzi wangu

Toa Maoni Hapa

SHIRIKISHA MWINGINE

Your email address will not be published. Required fields are marked *

SHIRIKI KUONGEZA MISTARI