MISTARI YA WIMBO HUU

Yeah, M-Lab

Naimani muda umefika niacheni nipige mishe
Dili za uhakika ka umeziba njia nipishe
Busara yahitajika majani yasiwadatishe
Mi ni kaka naheshimika amkeni niwaelimishe
Nataka mic moja wangoja nisababishe
MCs hawana adabu lazima niwaadabishe
Wenye mistari mbuzi wapuuzi niwahabarishe
Kaeni kando watoto wa juzi makuzi niwaelimishe
Machizi nwadatishe mitaa nipagawishe
Boy Stereo na yoyote usinilinganishe
Now naleta msiba sokada best wishes
Bora ujifanye hujui usijue nikuaibishe
Uwezo mpaji Mungu sema simu batilishe
Taarab imejaa majungu tega sikio uthibitishe
Mziki sio kamari fake emcee jisalimishe
Bongo tayari Uganda na Kenya kawafahamishe
Polepole ndo mwendo unipe nini niharakishe
Gazeti usinipe skendo copy nyingi nikuuzishe
Mfano nawajibisha nawavua niwahadhirishe
Nadhani wamelianzisha kaka mkuu nilihitimishe uone

Listen when I say it now
Listen when I say it now
Listen when I say it now
Listen when I say it now

Wanao-force kingi gogota wana-confess
Rest in peace dingi Dandu Vivi na Complex
Maadui hawaponi mbele ya komando Kipensi
Nawaza mpaka mtoni ubongo wangu hauna fence
What’s the difference kati yao wakali and I
Wana reference ukweli uko mbali they lie
Wapi mi kimziki soo kama eagle na-fly
Tatu point hauko-force sibadiliki ndo upae
Sharubu zimewachoma wanamkataa kambale
Utakufa ukianzisha noma mi na gun we una mshale
Wanaopenda lift hawastopishi hii Defender
Kama Mkwawa na-resist no retreat no surrender
Nawarusha maskani ka Nesta na Lucky Dube
Bara mpaka pwani namzuka wa Bi Kidude
Bongo na-reflect masista wana dudu
Sitegwi na mini-skirts sipandi vitax bubu
Uswazi nachapa kazi kama Daz ya manunda
Sinadi makazi nshaazima vazi napiga bunda
Ka unajipodoa kidume na demu who’s chick
Nawachokonoa kama vijiti vya toothpick

Listen when I say it now
Listen when I say it now
Listen when I say it now
Listen when I say it now

Naona watoto wadogo bado wanaichezea fasihi
Nasikia masharobaro wanajiita ma-emcee
Kwenye sanaa kitambo kama ukumbi wa DDC
Kabla ya club Mambo na station ya TBC
Rapper ka Moddy B Shirina Mori B
Sekunde tunauzima moto tipa is all I need
Mi natafuta money kwa nguvu na kwa bidii
Ile ilofanya watengane Mansuli na Hermy B
Ikiisha side A inageuzwa side B
Sina songs kama Trey kwenye game ya RnB
Usiige upate jina kama mchovu Gosby
Hamuwezi kupanga vina wabovu kama Izzo B
Nani anabisha ikitoka A inafuata B
Sa ruka na hii michoko inajivisha unabii
We sio vituliza vipago ka “Eno Mic” ya Ziggy Dee
Watafungasha virago na kusepa ka Madee
Maisha yangekuwa ya mkopo wangapi wange-clear madeni
Bongo inauzwa Gospel Madee mkumbusheni
Natema vyenye utata naacha blanks kama Bill
Wanajua kinachofuata nikishasoma Albadil

Listen when I say it now
Listen when I say it now
Listen when I say it now
Listen when I say it now

Listen when I say it now

Toa Maoni Hapa

SHIRIKISHA MWINGINE

Your email address will not be published. Required fields are marked *

SHIRIKI KUONGEZA MISTARI