MISTARI YA WIMBO HUU

Machoni kama watu mioyoni hawana utu
Imani imetoweka mabaya yanaongezeka
Machoni kama watu mioyoni hawana utu
Imani imetoweka mabaya yanaongezeka

Machoni kama watu mioyoni hawana utu
Imani imetoweka mabaya yanaongezeka
Machoni kama watu mioyoni hawana utu
Imani imetoweka mabaya yanaongezeka

Wengi wao wanatabasamu wanaongea kwa nidhamu
Wanajifanya watu wa karibu kumbe hao ndo sumu
Wameweka mbele dini fungo moyo usiwaamini

(Si unakumbuka alikufaa kwa dhiki)

Kweli

(Enzi zile upo nae marafiki)

Aha yuko wapi sasa hayupo tena ashasaliti
Kweli akufaae kwa dhiki mara nyingine ni msaliti
Alishatembea na mkeo kwa gia ya urafiki
Shoga yako kwako habanduki mmeo akakutaliki
Unajuta ye anacheka kwani ndoa keshaivuruga
Mmeo ametimua ye keshatawala nyumba
Baba na nyumba ndogo watoto wanalia mateso
Anadiriki hata kuwakana hana huruma hata kidogo
Haina mshangao watu wa aina hii wapo
Sio sehem zingine hata hapa ulipo wapo
Jirani yako mchana mnacheka usiku mwanga
Nia yake kuona life oh inapinda
Dili zote zigime mipango igonge mwamba afya yako
Bandika bandua ya magonjwa itatamba

Machoni kama watu mioyoni hawana utu
Imani imetoweka mabaya yanaongezeka
Machoni kama watu mioyoni hawana utu
Imani imetoweka mabaya yanaongezeka

Machoni kama watu mioyoni hawana utu
Imani imetoweka mabaya yanaongezeka
Machoni kama watu mioyoni hawana utu
Imani imetoweka mabaya yanaongezeka

Yoh
Dunia inavunda vvu walimwengu hawashikiki
Wengi wanapenda ngono lakini kuzaa hawataki
Wengi nacheka nao tu lakini sio kwa dhati
Hivyo ni kama nipo gizani halafu nalamba ncha ya mkuki
Wengi wanatoa mimba wengine wanatupa watoto
Ungekuwa wapi mama yako angekutupa enzi hizo
Imani hakuna ndani ya maovu yasio na mwisho
Nakata tamaa akili inachoka moyo mzito
Machoni kama watu kumbe wamejaa unyama tu
Kaa chonjo chunga sana napo akili kichwani tu
Hapendi kukuona unatesa juu yako mzigo chuki
Ameshatega mabaya mitego ndo haikamatiki
Hapendi kuona unawini hapendi kuona unafuraha
Raha yake kuona umezungukwa na karaha
Hana raha anapoona mambo safi kiuchumi
Moyo utakuwa shwari tu pale una hali duni

Machoni kama watu mioyoni hawana utu
Imani imetoweka mabaya yanaongezeka
Machoni kama watu mioyoni hawana utu
Imani imetoweka mabaya yanaongezeka

Machoni kama watu mioyoni hawana utu
Imani imetoweka mabaya yanaongezeka
Machoni kama watu mioyoni hawana utu
Imani imetoweka mabaya yanaongezeka

Huyo ndo mwanadamu anapowini tu dharau
Napo ni mgumu kuelewa mwepesi kusahau
Anajionyesha ana hurumampole na mkarimu
Na aliye mstari wa mbele kutoa ahadi tamu
Usimpa nafasi hata ajue zako habari
Hana jema chunga sana hana ujio wa heri
Hataki kabisa kuona unavuta hewa hii lakini
Wapi mipango inabaki zzz
Ni rahisi kwake kupata mali kwa njia ya kuua
Haya mambo hi hali nadhamni wote mnaijua
Mlale pema mliouwawa mkidai zenu haki
Sisi bado tupo duniani hatujui lini tamati
Jasho la mnyonge huwa ni neema kwa wachache
Ni kilio cha fukara chenye lengo haki nipate
Stuka huko tunakokwenda kunatisha
Kwani itakuwa ndoto watu kutenda mema kabisa

Machoni kama watu mioyoni hawana utu
Imani imetoweka mabaya yanaongezeka
Machoni kama watu mioyoni hawana utu
Imani imetoweka mabaya yanaongezeka

Machoni kama watu mioyoni hawana utu
Imani imetoweka mabaya yanaongezeka
Machoni kama watu mioyoni hawana utu
Imani imetoweka mabaya yanaongezeka

Toa Maoni Hapa

SHIRIKISHA MWINGINE

Your email address will not be published. Required fields are marked *

SHIRIKI KUONGEZA MISTARI