MISTARI YA WIMBO HUU

Nakupenda mpenzi wa maisha
Maisha maisha
Na mimi moyoni nna furaha tele moyoni
Kuwa wako mwenzi wa maisha
Katu hayatoisha toka moyoni mwangu
Nimekuchagua we uwe wangu
Vipingamizi vingi waliweka
Asante Mola tumevuka
Tupamoja sasa wenye kusema wacha waseme
Nakupenda wanipenda
Furaha twaidumisha
Nitakuwa wako maisha utakuwa wangu kabisa

Siku yangu imefika
Imefika ah aah
Na mimi moyoni nna furaha tele moyoni
Kukupata mwenzi wa maisha
Nami naahidi nitakupa vyote
Tangu sasa hata milele
Siku yangu imefika imefika ah aah
Na mimi moyoni nafuraha tele moyoni
Furaha furaha furaha tele moyoni
Furaha furaha furaha tele moyoni

Ee hee olala lala lala lalalaa
Oo hoo ooh uuiih
Uuh huu ulala lala lala
Aa haa uuh huu
Aa haa uuh huu
Wawa wawawa

Natoa machozi ya furaha
Furaha furaha
Kwani penzi letu limekwishaota mizizi
Umekuwa wangu laazizi
Nami naamini tutaishi sote
Tutapita na pande zote
Nimekuwa wako mahabuba
Kaeni kando acheni pupa
Tutapita kote pande zote mahali pote
Wenye kusema na waseme
Nakupenda wanipenda
Umekuwa wangu wa maisha wa
Maisha ah maisha
Mmh!

Ee hee ee hee
Ulala lala lala lalala
Ninalo penzi la milele
Moyoni mwangu
Ninatoa machozi ya furaha ah aa haa
Yee eh nina furaha
Ninalo penzi la milele
Ee hee aa haa
Mmhh!

Toa Maoni Hapa

SHIRIKISHA MWINGINE

Your email address will not be published. Required fields are marked *

SHIRIKI KUONGEZA MISTARI

VIDEO YA WIMBO HUU