MISTARI YA WIMBO HUU

Kazi yake Mola
Haina makosa
Kazi yake Mola
Haina makosa
Anafanya atakalo, anafanya awezalo
Kwani dunia ni yake na hukuna ashindwalo
Kazi yake Mola
Haina makosa
Kazi yake Mola
Haina makosa
Anafanya atakalo, anafanya awezalo
Kwani dunia ni yake na hukuna ashindwalo

Umekuta dunia imeandaliwa
Na we bila hiyana si ukazaliwa
Umekuta wasafiri (wasafiri)
Walotutoka kwaheri (kwaheri)
Kimwili haupo nasi, kiroho tupo nawe
Upo kwenye kina, kati mbao juu mawe
Mchana na usiku tunaomba tuwe nawe
Haiwezi kuwa sawa
Ugonjwa hutibika, mauti hayana dawa
Kwaheri Mwanahawa
Kizima huaribika, kufa na kupotea
Mchana na usiku dua tunakuombea
Ulale mahali pema huku unatungojea
Njia yetu ni moja ipo siku utatupokea
Salamu wasalimie wote utaowakuta
Waambie Babu Tale machozi kashafuta
Na kashalala matanga
Tangu enzi zile alizoondoka kichanga

Kazi yake Mola
Haina makosa
Kazi yake Mola
Haina makosa
Anafanya atakalo, anafanya awezalo
Kwani dunia ni yake na hukuna ashindwalo
Kazi yake Mola
Haina makosa
Kazi yake Mola
Haina makosa
Anafanya atakalo, anafanya awezalo
Kwani dunia ni yake na hukuna ashindwalo

Hii ni siri kubwa aloipanga Maanani
Hata Abdu Bonge siku yako haijulikani
Hata ukiwa na body kama producer Majani
Lazima utakwenda vyovyote inalazimu
Haina pa kujificha siku yako inapotimu
Tumuombee Mwanahawa yupo kwenye mustakimu
Awe na ufahari mwili ukiwa kuzimu
Umemuacha mpweke Ibra Modo anakuwaza
Kwani kila kukicha ye maswali anauliza
“Mjomba Idd, eti mama yuko wapi?”
Inabidi niongope huku sitaki
Naangaza pale mbele mama Tale analia
Pembeni namuona Kwembe Tolu na Lamia
Mbele yao ukungu
Futa machozi mama Dulla yote kazi ya Mungu
Jikaze kama mwanzo alivyoondoka Ally Zungu

Kazi yake Mola
Haina makosa
Kazi yake Mola
Haina makosa
Anafanya atakalo, anafanya awezalo
Kwani dunia ni yake na hukuna ashindwalo
Kazi yake Mola
Haina makosa
Kazi yake Mola
Haina makosa
Anafanya atakalo, anafanya awezalo
Kwani dunia ni yake na hukuna ashindwalo

Naomba mnisamehe kuomboleza nimechoka
Namuona mwarabu sa machozi yanamtoka
Sio kosa lake bali ye anauchungu
Nawaza ndugu zake Mwanahawa na Ally Zungu
Usiwe na wasiwasi wamefika mbele ya haki
Kifo ni desturi wanadamu hatunyimiki
Salamu Kwakwe Chupu, utaendesha kila kitu
Ndege gari we utaweza
Ila siku ya mwisho tutakubeba kwenye jeneza
Na watu msururu
Hapa Msola, Eddy Donoa pembeni mama Lulu
(Rest in peace, pumzika kwa amani)

Kazi yake Mola
Haina makosa
Kazi yake Mola
Haina makosa
Anafanya atakalo, anafanya awezalo
Kwani dunia ni yake na hukuna ashindwalo
Kazi yake Mola
Haina makosa
Kazi yake Mola
Haina makosa
Anafanya atakalo, anafanya awezalo
Kwani dunia ni yake na hakuna ashindwalo

Toa Maoni Hapa

SHIRIKISHA MWINGINE

Your email address will not be published. Required fields are marked *

SHIRIKI KUONGEZA MISTARI