MISTARI YA WIMBO HUU

Kweli mapenzi matamu lakini ninaugua aah
Mbona unanipa wazimu kwa kunisumbua aah
Ulinituma sambusa na vile bagia aah
Cha ajabu ukasusa na ukanitupia aah
Mama kijacho unavisa na mwenyewe sielewi kwanini
Nikiwa sipo unacheka, nikirudi unaninunia nini
Unataka supu ya ngamia nitaipataje eh
Nikikosa wewe unaumia nitafanyaje eh

Ni kweli ulinituma udongo, na mimi nikakosa aah
Ukaniletea londo na ndani nikawekwa
Ni kweli ulinituma udongo, na mimi nikakosa aah
Ukaniletea londo na ndani nikawekwa

Mama we kija mama
Mbona unanivuruga
Vururu vururu vururu
Mbona unanivuruga
Mama we kija mama
Mbona unanikoroga
Kororo kororo kororo
Mbona unanikoroga
Mama kija mama, mwenzako nakosa raha sana
Nkirudi nachoka na visa unavyonifanyiaga

Mamaa mama ohh
Mama kija mama
Mbona unanikoroga
Kororo kororo kororo
Mbona unanikoroga

Hata kama nikikosa kula unaleta zogo
Yaani nyumbani amani hakuna umekuwa

Mbogo
Usiku unataka nikupepe
Feni si lipo lakini mwenzangu lazima unitese
Haloo
Usiku unataka nikupepe
Feni si lipo lakini mwenzangu lazima unitese

Ila dosalale leo umenifanya nisilale
Mwenzako nakonda na penzi la sasa nalimiss

Penzi la muda ule
Ila dosalale leo umenifanya nisilale
Mwenzako nakonda na penzi la sasa nalimiss

Penzi la muda ule

Nyumbani daily makelele
Mapenzi hakuna kama yale
Mawazo mengi unanipa wewe
Mapenzi yananifanya nisilale
Nyumbani daily makelele
Mapenzi hakuna kama yale
Mawazo mengi unanipa wewe
Mapenzi yananifanya nisilale

Mama we kija mama
Mbona unanivuruga
Vururu vururu vururu
Mbona unanivuruga
Mama we kija mama
Mbona unanikoroga
Kororo kororo kororo
Mbona unanikoroga
Mama kija mama, mwenzako nakosa raha sana
Nkirudi nachoka na visa unavyonifanyiaga

Mamaa mama ohh
Mama kija mama
Mbona unanikoroga
Kororo kororo kororo
Mbona unanikoroga

Na unalalamika kichefu chefu
Unataka embe tena ng’ong’o
Unakuja na nyundo unitoe jino
Eti baby unapendeza na pengo

Huyoo, kochi lipo lakini unataka kupakatwa
Umetoa mpya umekumbuka shule na

Unatamani kuchapwa

Mama we kija mama
Mbona unanivuruga
Vururu vururu vururu
Mbona unanivuruga
Mama we kija mama
Mbona unanikoroga
Kororo kororo kororo
Mbona unanikoroga

We unatakaje mbona vururu vururu
Mbona unanivuruga
We unasemaje mbona kororo kororo
Mbona unanikoroga
We unatakaje vururu vururu
Mbona unanivuruga
We unasemaje kururu kururu
Mbona unanivuruga

Baby unataka ghorofa, umechoka nyumba za chini wee
Eti nunua Verossa uende nayo clinic
Baby unaniboa, Chambusa unamkoroga
Babu Tale umemboa, baba Ubaya umemkoroga
Fella umemboa, Baraka Saddy umemkoroga
Tatu Meme umemboa, Abdu Mwinyi

Umemkoroga
Issa baba umemboa, Chief Kiumbe umemkoroga

Toa Maoni Hapa

SHIRIKISHA MWINGINE

Your email address will not be published. Required fields are marked *

SHIRIKI KUONGEZA MISTARI

VIDEO YA WIMBO HUU