MISTARI YA WIMBO HUU

Mama yangu (yangu)
Wewe ni nguzo maishani mwangu (mwangu)
Taa imulikayo mbele yangu (yangu)
Daima milele wewe
Ni mama yangu (yangu)
Wewe ni nguzo maishani mwangu (mwangu)
Taa imulikayo mbele yangu (yangu)
Mawazo yako mama yanaongoza maisha yangu oh

Ni tuzo gani unayostahili
Wa kuweza oh kuthamini
Shida zangu oh usumbufu wangu
Toka kuzaliwa kwangu
Na mpaka leo nasimama mbele yako mama
Unastahili sifa kwa mapenzi uliyoonyesha kwangu
Tangu nazaliwa mama yangu wo uwo
Oh oh

Mama yangu (yangu)
Wewe ni nguzo maishani mwangu (mwangu)
Taa imulikayo mbele yangu (yangu)
Daima milele wewe
Ni mama yangu (yangu)
Wewe ni nguzo maishani mwangu (mwangu)
Taa imulikayo mbele yangu (yangu)
Mawazo yako mama yanaongoza maisha yangu oh

Umenilea tangu nazaliwa
Haukuchoshwa na wangu usumbufu
Muda wako mwingi mama uliutumia
Kwa ajili yangu oh asante mama
Unastahili sifa kwa mapenzi ulioonyesha
Tangu nazaliwa oh mama yangu
Asante sana mama oh
Oh oh

Mama yangu (yangu)
Wewe ni nguzo maishani mwangu (mwangu)
Taa imulikayo mbele yangu (yangu)
Daima milele wewe
Ni mama yangu (yangu)
Wewe ni nguzo maishani mwangu (mwangu)
Taa imulikayo mbele yangu (yangu)
Mawazo yako mama yanaongoza maisha yangu oh

Nikikumbuka mema ulonifundisha
Nikikumbuka mabaya ulonikataza
Nashindwa jinsi hata ya kuelezea
Mafunzo yako ndio nguzo kwangu mama
Nikisema nikulipe
Itanigharimu maisha yangu yote
Nikisema nikuzawadie
Sioni kile unachostahili
Ninachoweza sema nakupenda sana mama
Nakushukuru kwa mema yote uliotenda kwangu

Mama yangu (yangu)
Wewe ni nguzo maishani mwangu (mwangu)
Taa imulikayo mbele yangu (yangu)
Daima milele wewe
Ni mama yangu (yangu)
Wewe ni nguzo maishani mwangu (mwangu)
Taa imulikayo mbele yangu (yangu)
Mawazo yako mama yanaongoza maisha yangu

Toa Maoni Hapa

SHIRIKISHA MWINGINE

Your email address will not be published. Required fields are marked *

SHIRIKI KUONGEZA MISTARI

VIDEO YA WIMBO HUU