MISTARI YA WIMBO HUU

Bongo movie, Bongolala, Bongo muziki
Taaluma isiyo vigezo na ubongo hautumiki
Taaluma taa ya kichwa, taa ya Umma
Nkurumah chuo kikuu, I know I knew
Maria mama Manuu, haina usamaria bahari aloweka miguu
Harakati magirini, sikumbisi Mr. II
Kwenye moto hakuna madini, joto one two watu
Midundo ni mandugu DIG, miondoko BIG
Uasili ni mia, hapa jadi siuachii
Nakuumizia umbali mrefu sana, shindachi power
Nguvu ufahamu, let me MC sawa
Ni tiba tibia hawa wana wa Adam na Hawa
New school, old school masantula (new school, old skul masantula!)
Kizamani kisasa, samba Mapangala (kizamani kisasa, samba Mapangala)
Jyeah
Nifiche kweli, mishe wangu wa pale kitaani ni la hasha
Siku hizi hakuna kazi za wito
Nyimbo nyingi hazina pumzi ya kumaliza intro ghetto
Joh Manuva wa Mandugu Digi.. dunga za moto

Leta manuva, leta manuva
Leta manuva, leta manuva
Joh Manuva wa Mandugu Digi.. dunga za moto
Leta manuva, leta manuva
Leta manuva

Jhea
Mi naleta emotional kwenye rap shinda hawa best singers
Nusu mtu nusu muujiza kitu gani sina
Machizi, tinga
Weusi, jina
Arusha, jina
Ukweli ndo safina
Wapi wanangu wa unga limited
Wananiita zungu la flow, unlimited
Heko Sinoni mpaka Keko, nipeni toka Metro
Kitambo ni za moto, zikiwaunguza
Babylon system ngoma ni ngumu, ngumu
Huu mwenendo vipi chama kidumu
Kama hukumjali daktari, vipi hawa maaskari
Basi na hii wekeni wazi kwamba rushwa ni halali
Kumi na nane mkibana nazifungia mbali
Mimi ni nani sio kazi yangu kaulize mitaani
Mishahara haitoshi that’s why
Mnaendesha ng’ombe weusi sio makhsai
Sifungulii milango stress mbona mtafurahi
Biashara na mambo za kujuana ndo haifai
Mapigo is on the menu bye bye
Msikatiki soma yenu nai nai

Leta manuva, leta manuva
Leta manuva, leta manuva
Joh Manuva wa Mandugu Digi.. dunga za moto
Leta manuva, leta manuva
Leta manuva

Kiutu uzima hampotezei ngoma kali za machizi
Ni maigizo mlikuwa busy kwa upuuzi mnao-release
Ji-squeeze halafu freeze gwara kwa mwanangu Izzy
Ni baraka pande hizi, asante zote kwa Mwenyezi
Ah na-change flow kama bureau ei ei
Hizi ndo zile mnakeshaga mkiomba kona hazitokei
Ninazo nyingi kama mkwanja kwenye akaunti ya Mengi
Planet hakuna usalama, Bongo naisomea UK
Kimsingi sijaishi kwingi kama mengi niliyoyaona
Toka mtaa niliozaliwa pale jobless corner
Nashindwa kuelewa mnapokosa vya kuchana
Na kwa hii mafanikio si mswahili kuwa stunner
Na misimu huishtukii, hujui ni summer?
Joh niko na pensi, show zangu nyeusi
Ndo hurusha mabinti fence
Na midungo ndani ya club, ni ma bboy stance
I’ll be chilling in the club with my bboy stance

Leta manuva, leta manuva
Leta manuva, leta manuva
Joh Manuva wa Mandugu Digi.. dunga za moto
Leta manuva, leta manuva
Leta manuva

Dunga utawaua
My condolences

Toa Maoni Hapa

SHIRIKISHA MWINGINE

Your email address will not be published. Required fields are marked *

SHIRIKI KUONGEZA MISTARI