MISTARI YA WIMBO HUU

Nimeshasema mapenzi na wewe basi
Nikisema basi tena staki
Yaani mapenzi na dhiki
Wapi na wapi
Sijavaa nguo mpya mwaka wa ngapi
Nimeshasema mapenzi na wewe basi
Nikisema basi tena staki
Yaani mapenzi na dhiki
Wapi na wapi
Sijavaa nguo mpya mwaka wa ngapi

Sio siri mi nakuthamini
Nini hautaki we kuwa na mimi
Si unajua kipato changu cha chini
Isiwe sababu ya kuniacha mimi
Umasikini wangu sijapenda
Ila nenda mama nenda
Japo moyoni sijapenda
Ila ruksa mama nenda unapokwenda
Najua sababu umaskini umeamua kuniacha mimi
Kumbuka we ulikuwa yamini
Ukaapa kwa Mungu huniachi mimi
Japo unasema sijafanya jema
Sema mama sema
Umeamua kunisema ushanisema sana mwisho umenitema

Nimeshasema mapenzi na wewe basi
Nikisema basi tena staki
Yaani mapenzi na dhiki
Wapi na wapi
Sijavaa nguo mpya mwaka wa ngapi
Nimeshasema mapenzi na wewe basi
Nikisema basi tena staki
Yaani mapenzi na dhiki
Wapi na wapi
Sijavaa nguo mpya mwaka wa ngapi

Miaka mingi imepita mi napata tabu
Sijapata raha kutwa kucha ni ghadhabu
Kitendawili cha muda sijapata jibu
Upendo wangu wa dhati ndo unaniadhibu
Shida mateso karaha vinazidi nichanganya
Siku inapita mimi sijala
Ndo sababu mi naondoka
Shida mateso karaha vinazidi nichanganya
Siku inapita mimi sijala
Ndo sababu mi naondoka

Iih (nakuomba vumilia)
Yote (ni matatizo ya dunia)
Muombe Mungu atakusaidia
Kweli mi na nia
Dear nionyeshe njia

Nimeshasema mapenzi na wewe basi
Nikisema basi tena staki
Yaani mapenzi na dhiki
Wapi na wapi
Sijavaa nguo mpya mwaka wa ngapi
Nimeshasema mapenzi na wewe basi
Nikisema basi tena staki
Yaani mapenzi na dhiki
Wapi na wapi
Sijavaa nguo mpya mwaka wa ngapi

Nakuomba mama usiondoke
Nirudi home tuishi wote
Si umesema shida na raha tuwe wote
Sasa vipi leo unataka uondoke
Mamii mamii (mami mami)
Mamii mamii
Mamii mamii (mami mami)
Mamii mamii

Toa Maoni Hapa

SHIRIKISHA MWINGINE

Your email address will not be published. Required fields are marked *

SHIRIKI KUONGEZA MISTARI

VIDEO YA WIMBO HUU