MISTARI YA WIMBO HUU

Kisa wewe masikini waona huwezi kuwa nami
Marafiki wanahoji kwamba we utanipa nini
Jibu lao ni moja, kwamba nahitaji penzi
Bila shaka ni la dhati, lisije leta mauti
Kisa wewe masikini waona huwezi kuwa nami
Marafiki wanahoji kwamba we utanipa nini
Jibu lao ni moja, kwamba nahitaji penzi
Bila shaka ni la dhati, lisije leta mauti

Uuh yeah, nafurahi
Nafurahi kuwa nawe, hilo nataka uelewe
Kwamba mapenzi ni ya wawili
Nafurahi kuwa nawe, hilo nataka uelewe
Kwamba mapenzi ni ya wawili

Wewe kwangu ndio mfalme
Wewe kwangu ndio mfalme
Nifanye niwe kwako wako malikia
Kwa penzi lako naahidi kukutumikia
Nifanye niwe kwako wako malikia
Kwa penzi lako naahidi kukutumikia
Sihitaji mwewe kuja kunichukulia
Walimwengu wana mengi, mimi sitoyasikia
Mpenzi wangu nakupenda, nimeziba masikio

Nafurahi kuwa nawe, hilo nataka uelewe
Kwamba mapenzi ni ya wawili
(Ya wawi– ya wawi– ya wawili)
Nafurahi kuwa nawe, hilo nataka uelewe
Kwamba mapenzi ni ya wawili
(Ya wawi– ya wawi– ya wawili)
Nafurahi kuwa nawe, hilo nataka uelewe
Kwamba mapenzi ni ya wawili
(Ya wawili)
Nafurahi kuwa nawe, hilo nataka uelewe
Kwamba mapenzi ni ya wawili
(Ya wawi– ya wawi– ya wawili)

Toa Maoni Hapa

SHIRIKISHA MWINGINE

Your email address will not be published. Required fields are marked *

SHIRIKI KUONGEZA MISTARI