MISTARI YA WIMBO HUU
Mapenzi yangu yaweke
Usiyatoe asilani
Mapenzi yangu yaweke
Usiyatoe asilani
Penzi lina raha yake
Asiyejua ni nani
Penzi lina raha yake
Asiyejua ni nani
Penzi mfano wa pete
Uvaapo kidoleni
Penzi mfano wa pete
Uvaapo kidoleni
Mapenzi matamu
Niwapo nawe mpenzi
Sioni mwingine
Wa kufanana na wewe
Nitalienzi penzi lako
Sitokuacha asilani
Nitalienzi penzi lako
Sitokuacha asilani
Mpenzi usiwe na shaka
Nakupenda kwa yakini
Mpenzi usiwe na shaka
Nakupenda kwa yakini
Wala sitobadilika
Hilo ujue yakini
Wala sitobadilika
Hilo ujue yakini
Mwingine sitomtaka
Hilo kaa ubaini
Mwingine sitomtaka
Hilo kaa ubaini
Mapenzi matamu
Niwapo nawe mpenzi
Sioni mwingine
Wa kufanana na wewe
Nitalienzi penzi lako
Sitokuacha asilani
Nitalienzi penzi lako
Sitokuacha asilani
Pendo tutalifaidi
Apendapo Lakhmani
Pendo tutalifaidi
Apendapo Lakhmani
Wala hapiti fisadi
Kuvunja yetu hisani
Wala hapiti fisadi
Kuvunja yetu hisani
Na mi ninakuahidi
Sitokuacha asilani
Na mi ninakuahidi
Sitokuacha asilani
Mapenzi matamu
Niwapo nawe mpenzi
Sioni mwingine
Wa kufanana na wewe
Nitalienzi penzi lako
Sitokuacha asilani
Nitalienzi penzi lako
Sitokuacha asilani
Penzi langu ninakupa
Uliweke moyoni
Penzi langu ninakupa
Uliweke moyoni
Usije ukalitupa
Nikasumbuka duniani
Usije ukalitupa
Nikasumbuka duniani
Huenda nikabwie chupa
Nitoweke duniani
Huenda nikabwia chupa
Nitoweke duniani
Mapenzi matamu
Niwapo nawe mpenzi
Sioni mwingine
Wa kufanana na wewe
Nitalienzi penzi lako
Sitokuacha asilani
Nitalienzi penzi lako
Sitokuacha asilani
Mapenzi matamu
Niwapo nawe mpenzi
Sioni mwingine
Wa kufanana na wewe
Nitalienzi penzi lako
Sitokuacha asilani
Nitalienzi penzi lako
Sitokuacha asilani
No comments yet