MISTARI YA WIMBO HUU

Naona mama analia, na mi ndo namchadazia
Mama anakuombea sana anategemea uje kumsaidia
Nilitakiwa niwe nimekufa, but nah lakini wapi
Waganga watakushusha, Mungu ananipaisha
Niko hai kwa sababu so usinitaftie sababu
Mnataka mnione hivi hivi mpaka nikiwa babu
Malengo yangu yapo pale pale, sibadilishi
Kufanya kazi kwa bidii maisha mazuri niishi
Na mambo mengi nimeona, maadui nakumbuka
Wengi hawakuwa na mimi wakati nataabika
Nahangaika huku na kule wakati namoka
Ni kipindi cha mapito wala usitie shaka
All eyes on Lord Eyes, nani mwingine
Mshanilambazia sana sasa kipi kingine
Kesi mbili tatu nne hazitoshi nipeni nyingine
Mtoto wa Mungu ukimkandamiza unamjaribu yeye si mwingine

Huku na kule sina mashaka (sina mashaka)
Huku na kule sina mashaka usitie mashaka (mashaka)
Haya ni mapito tu (mapito mapito)
Haya ni mapito tu (mapito tu)
Huku na kule sina mashaka (sina mashaka)
Huku na kule sina mashaka usitie mashaka (mashaka)
Haya ni mapito tu (mapito mapito)
Haya ni mapito tu (mapito tu)

Nafurahi kwa kuwa ni siku mpya
Naona alama ya ushindi nani hataki kushikika
Lord Izzy eeh, Lord Izzy aah
Naona alama ya ushindi nani hataki kuzishika
Na msijifanye hamjui, haa hamjui
Mkijifanya hamjui, haa hamtujui
Haya maneno kwenye mitandao mi hayanisumbui
Mnaongea vitu hamvijui, hee hamvijui
Kama mi sio binadamu ina maana sikui
Mwili wangu umekuwa hekalu sasa hamnitungui
I’ve got God with me and he’s guarding me
Mbona siwaelewi mko na mimi au hamjui
Maana naona bora peke yangu rafiki wa kweli simjui
Wale wanao act act kama binti
Silishani nao aan aah hata bit
Virungu na pingu bado mnanitia kiwingu

Huku na kule sina mashaka (sina mashaka)
Huku na kule sina mashaka usitie mashaka (mashaka)
Haya ni mapito tu (mapito mapito)
Haya ni mapito tu (mapito tu)
Huku na kule sina mashaka
Huku na kule sina mashaka usitie mashaka (sina mashaka)
Haya ni mapito tu (haya)
Haya ni mapito tu (haya ni mapito tu)

Mungu mbariki Ray C, mbariki na mama yake
Mtoe kwenye haya majanga, mrudishie maisha yake
Enhe niambie, okay lete habari
Lord Izzy kafanya hivi na hivi, uzeni hiyo habari
Eh Mungu nibariki niepukane na hii hali
Too many fake people eeh, wamecheka aa
Naziona dimples, nini ndo power window
Napata nikiuza hindo, F ndo power window
(The boy is innocent!)
Naingizwa kwa majanga na sijala hata senti
Visanga na majungu, mnataka kugusa macho ya Mungu
Virungu na pingu bado mnanitia kiwingu

Huku na kule sina mashaka (sina mashaka)
Huku na kule sina mashaka usitie mashaka (mashaka)
Haya ni mapito tu (mapito mapito)
Haya ni mapito tu (mapito tu)
Huku na kule sina mashaka
Huku na kule sina mashaka usitie mashaka (mashaka)
Haya ni mapito tu (mapito tu)
Haya ni mapito tu (oh oh)

Toa Maoni Hapa

SHIRIKISHA MWINGINE

Your email address will not be published. Required fields are marked *

SHIRIKI KUONGEZA MISTARI